|  | 
| RAIS WA NIGERIA GOODLUCK JONATHAN . | 
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amezungumza wazi kwa mara ya kwanza kuhusu kutekwa kwa waschana takriban 200 wa shule kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Katika taarifa yake ya kwanza hadharani tangu wasichana 200 kutekwa nyara na 
watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Waislamu wenye itikadi kali wa Boko Haram, 
Rais Goodluck Jonathan, amesema kuwa kila juhudi zinapaswa kufanywa kuwakomboa 
wasichana hao.
Tangazo la Rais lilitolewa kufuatia shinikizo zilizotolewa na familia, 
makundi ya wanawake na watu wengine ambao wameitaka Serikali kufanya bidii zaidi 
kuhakikisha kuwa wasichana hao wanakombolewa.
Rais alisema kuwa maafisa wa usalama wamekuwa wakitafuta kila mahali 
wakitumia ndege na helikopta lakini akakiri kuwa hawajafaulu kutambua 
walikofichwa wasichana hao.
Alisema kuwa Serikali yake imelazimika kuomba msaada katika kuwatafuta 
wasichana hao kutoka Serikali za Marekani, Uingereza na Uchina.
Jeshi la Nigeria limekuwa likipambana na kundi hilo la wapiganaji tangu mwaka 
2009, lakini mashambulizi na milipuko ya mabomu yameendelea kusikika kila mahali 
bila kukoma.
Hivi majuzi kumekuwa na milipuko katika mji mkuu wa Abuja katika muda wa 
majuma matatu ambapo karibu watu 90 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Mnamo Jumatano Kongamo la Dunia juu ya Uchumi wa Afrika utafanyika mjini 
Abuja na swala la usalama limewatia maafisa wa usalama tumbo joto, ambapo 
imetangazwa kuwa siku hiyo shule zote na afisi za Serikali zitafungwa ili 
kuimarisha usalama eneo hilo la mkutano
 
 
 
Post A Comment: