UMATI WA WATU KATIKA BARA BARA YA KENYATTA HAPA WAKISHUHUDIA FOLENI YA MAGARI
NI BAADA YA KARANDINGA KUSABABISHA AJALI.
Fatilia kwa karibu picha hizo ambazo tumezipata kwa hisani ya Blogu ya G. Sengo.

Jana jioni wakazi wa jiji la Mwanza wamepata usumbufu mkubwa mara baada ya barabara muhimu ya Kenyata kufungwa kwa muda katika muda mbaya wa kurejea kutoka makazini mara baada ya karandinga la jeshi la polisi lenye namba za usajili STG 9263 lililokuwa likitokea mahakamani kuelekea gereza la Butimba, likiwa na mahabusu kusababisha ajali mara baada ya kupoteza uelekeo .

Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa  karandinga hilo lilipoteza uelekeo mara baada ya kukata dif ile hali likiwa katika mwendo kasi hivyo likaibamiza kwa nyuma gari lililokuwa mbele yake aina ya Toyota Dutsun yenye namba za usajili T387 AAH, gari ambalo lilipoteza uelekeo na kuvagaa moja kati ya maduka kwenye barabara hiyo linalotazamana na kituo cha mafuta. 

Ajali hiyo imesababisha moja kati mahabusu waliokuwa kwenye karandinga hilo aliyekuwa na majeraha ya kuvunjika kwenye moja ya matukio ya kesi inayomkabili kuteguka zaidi huku wengine wakisalimika kwa muweza kujimudu kukamata sehemu za vishikio vya karandinga hilo wakati ajali ikitokea.

Uhaba wa kutokuwa na gari la ziada kubebea mahabusu limeligharimu jeshi la polisi mkoa wa Mwanza leo kwa jeshi hilo kutumia magari yake ya doria ya kawaida (Defender) kufaulisha wafungwa kwa makundi hali ambayo ilibidi zoezi hilo kutumia muda  mrefu kukamilika.

Pic up aina ya Toyota Dutsun  T387 AAH ikiwa imenasa kwenye moja ya maduka mara baada ya kugongwa na karandinga hilo la mahabusu.

Utaratibu wa kufaulisha mahabusu ukiendelea kufanywa na kikosi cha kuzuia vurugu FFU jeshi la polisi Mwanza.


Usalama ulizingatiwa na wananchi walikatazwa kulifikia eneo la tukio umbali wa mita 100.

Kasheshe ya msongamano barabara ya Kenyata jijini Mwanza.

Fundi akijaribu kuweka japo sawa kwa muda ili karandinga hilo lipate kuondoshwa eneo hilo kuondoa usumbufu wa kuziba njia ya barabara hiyo muhimu....

Si suala la kubeza twahitaji kuboresha vitendea kazi jeshi la polisi nchini kwani ipo siku yatazuka makubwa kuliko hili lililotokea hapo jana.
Axact

Post A Comment: