Kufanya makubwa zaidi  2015.
Na : Afisa Habari RS Mwanza.
MAAFISA WA SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA WAKIWA KATIKA MOJA YA ZIARA WILAYANI KUKAGUA MAENDELEO YA SHUGHULI MBALI MBALI ZA SERIKALI.
Mkoa wa Mwanza umeshika nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne yaliyo tangazwa hivi karibuni kwa kupata ufaulu wa GPA 2.67, huku ukitanguliwa na Mkoa wa Pwani (GPA 2.79) na Shinyanga (GPA 2.69) haya  yamebainishwa na Afisa Elimu Taaluma katika Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza Mwl. Gervas Sezulu wakati wa mahojiano baina yake na Mtandao huu wa Mkoa.
Sezulu amesema, ufaulu huo unaifanya Mwanza kuwa moja ya Mikoa inayofikia malengo ya Mpango wa matokeo makubwa sasa yaani Big Results Now (BRN). “Mwishoni mwa mwaka jana (2014), mitihani ya kidato cha nne ilifanyika nchini kote na Mkoa huu wa Mwanza ukiwa ni mmoja wapo shule zetu zote ” alisema Sezulu na kuongeza kuwa, kwa Mkoa wa Mwanza jumla ya wanafunzi 19,783 waliandikishwa kufanya mtihani huo, walifanya mtihani huo.
Amesema, kwa matokeo ya mwaka 2013 ya mtihani huo wa kidato cha nne, Mkoa wa Mwanza ulishika nafasi ya 12 kwa kupata ufaulu wa asilimia 39.29 hali hiyo ulifanya Mkoa kujipanga vizuri zaidi na huku ukijiwekea mikakati kabambe itakayo wawezesha kufanya vizuri zaidi kwa mwaka 2015.
Akibainisha mikakati hiyo, Sezulu alisema ni pamoja na kuendelea kuwathamini walimu, kuendesha na kutoa semina kwa walimu wote Mkoani hapo, kufanya mikutano na viongozi wa Elimu wilaya, kuwa na mpango kazi wa ufatiliaji wa karibu katika ngazi zote, kutoa majaribio yakutosha kwa watahiniwa wote, pamoja na kuwashirikisha wadau wa elimu kuhusu mafanikio yanayo patikana katika Mkoa wa Mwanza.
Mkoa wa Mwanza ambao unatekeleza mpango wa BRN uliowekewa wastani wa ufaulu wa kufikia silimia 70 ya kitaifa hali ambayo imeufanya Mkoa huo kubuni mbinu mbali mbali za kuuwezesha kushika nafasi za juu kitaifa miongoni mwa mikoa 27 ya Tanzania, ambapo 25 kwa Tanzania bara na miwili Tanzania visiwani.
Mbali na matokeo ya kidato cha nne, Sezulu alisema mafanikio hayo yamefikiwa kutokana na ushirikiano mzuri ulipo baina ya Walimu, wazazi pamoja na wanafunzi wenyewe ambao kwa namna moja wameonekana kujituma zaidi katika masomo yao.
Mbali ya matokeo ya kidato cha nne, Mkoa wa Mwanza umeonekana kufanya vizuri katika elimu ya msingi  kwa mwaka wa 2014, kwakuwa katika mtihani wa kumaliza darasa la saba Mkoa ulishika nafasi ya tatu kitaifa kwa kupata ufaulu wa asilimia 69.07 huku ukitanguliwa na Mkoa wa Dar es Salaam ambao katika matokeo ya darasa la saba ulipata ufaulu wa asilimia 77.94 na Kilimanjaro asilimia 69.08.
Hata hivyo Sezulu amesema wamejizatiti kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi katika mitihani ya mwaka huu wa 2015 kwa ya Shule ya msingi lakini pia Sekondari
Axact

Post A Comment: