Na Afisa habari RS- Mwanza
MKUU WA WILAYA YA SENGEREMA MH. ZAINAB TERACK, AKIHUTUBIA KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAJI KIMKOA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA MWANZA WILAYANI SENGEREMA. |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo amewataka wahandisi wa
miradi ya Maji katika Mkoa na wale wa Halmashauri na
miji midogo mkoani hapa kusimamia vizuri miradi ya maji na kwamba fedha zitakazotumika
kwenye miradi hiyo zitumike vizuri ilikusaidia kukamilika katika viwango vinavyotakiwa.
Akizungumza kwa kwenye kilele cha maji
mkoani hapa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Magesa Mulongo, Mkuu wa Wilaya ya
Sengerema, Zaibabu Terack kwenye sherehe
za kilele cha maji zilizofanyika Wilaya ya Sengerema, Mulongo alisema kuwa
miradi ya maji Mwanza inaweza kukamilika kwa wakati kama fedha za miradi hiyo
zitatumika vizuri.
Alisema kazi ya kusimamia miradi hiyo inapaswa kufanywa na wakandarasi
wa Halmashauri na miji midogo ambayo inapitiwa na miradi hiyo na kwamba kama
fedha za miradi zitatumika kinyume Mwanza itaendelea kuwa na tatizo la maji.
Katibu Tawala msaidizi maji, Wariba Sanya akitoa taarifa ya hali ya maji na miradi itakayo Tekelezwa Mkoani Mwanza. |
“Naomba niwaombe Wakandarasi wa maji kutoka Halmashauri zote za Mwanza
pamoja na miji midogo ambayo inapitiwa na miradi ya maji isimamie vizuri miradi
hiyo.Nataka kuona fedha za miradi zinatumika vizuri na miradi yote inatekelezwa
kwa wakati,”alisema Mulongo na kuongeza:
“Kama tutakwenda kinyume na matumizi ya fedha za miradi ya maji
tutaendelea kuwa na tatizo la maji na kero za maji ambazo zinawakabili wananchi
zitaendelea, hivyo sitakubali kuona wananchi wanateseka kwa kukosa maji wakati
Serikali yao inawajali kwa kuwaletea miradi ya maji.”
Akisoma taarifa ya miradi ya maji, Katibu tawala msaidizi maji Sekretarieti
ya Mkoa wa Mwanza, Warioba Sanya, alisema Serikali imewekeza Sh.84.46
bilioni kwa ajili ya miradi ya Maji ya mkoa wa Mwanza kupitia mapango wa maji wa (WSDP).
“Mwanza tunaishukuru Serikali, kwani licha ya kutupa miradi mbalimbali
ya maji Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya maji vijijini 217 kati ya hiyo
miradi 140 imekamilika sawa na asilimia 65 na kwamba miradi iliyobaki
itakamilika ifikapo mwezi juni mwaka huu,”alisema Sanya.
Mkoa wa mwanza kwa hivi sasa unawapatia maji wananchi kwa asilimia 61.
Post A Comment: