WAZIRI WA VIWANDA NA UWEKEZAJI CHARLES MWIJAGE WAKATI WA MKUTANO ULIOANDALIWA NA WAKALA WA VIPIMO NCHINI, HAPA ALIKUWA AKIJIBU BAADHI YA HOJA ZA WAJUMBE WA MKUTANO HUO
MKUU WA WILAYA YA MSOMA, HAMPHREY POLE POLE WAKATI AKICHANGIA JAMBO KWENYE MKUTANO HUO, POLE POLE ALIMWAKILISHA MKUU WA MKOA WA MARA MAGESSA MULONGO.
PICHA YA PAMOJA NA WAZIRI ALIYE KETI WANNE KUTOKA KUSHOTO WALIOKETI AKIWA NA WAKUU WA MIKOA ILIYO HUSIKA KATIKA MKUTANO HUO.
 
Na: Atley Kuni- Mwanza

Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji Charles Mwijage, amesema hayupo tayari kurudi kwenye makongamano, semina wala warsha ambazo hazina tija kwa manufaa kwa mustakabali wa zao la pamba nchini na badala yake amesema, kuanzia hivi sasa nguvu itaelekezwa kwenye utendaji zaidi ili kuleta matokea chanya kwa zao hilo ambalo lilikuwa mkombozi wa mkulima wa Tanzania katika miaka ya nyuma.

Mwijage ametoa kauli hiyo Jijini Mwanza wakati wa kongamano la wadau wa Sekta ya Pamba lililokutana Jijini humo kwa lengo la kujadili suala la vipimo sahihi kwa biashara endelevu ya zao la Pamba, “ Kuanzia sasa nimesema nimesikia kilio cha wadau, na nimeelewa lugha wanayo itaka sasa na mimi sipo tayari kuona makongamano na semina ambazo wenzetu wa Bodi ya Pamba wamekuwa wakiziitisha kila mwaka bila kuwa na matokeo chanya zinaendelea ” amesema Mwijage na kuongeza “lakini pia niseme kuna baadhi ya mambo ambayo yameongelewa hapa nadhani kama waziri mwenye dhamana nitayachukua nakwenda kuyafanyia kazi kwa yale yaliyo katika ngazi inayo nihusu.

Kauli ya Mwijage ilikuja mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Harrison Mtaka, kuitupia lawama bodi ya Pamba nchini, kuwa, imekuwa ikiendesha makongamano na warsha kwa wadau wa Pamba kila mwaka bila mafanikio, Mtaka katika maelezo yake alianza kwakusema “kama tunataka mabadiliko kwenye sekta ya Pamba lazima yawepo mabadiliko na kama ni suala la mabadiliko nilazima makongamano ya Bodi ya Pamba nchini yafutwe, kwani mamlaka hiyo haina Bodi ya wakurugenzi kwa zaidi ya miaka mitano (5), alisema mtaka na kuongeza  “Inashangaza  kila mwaka wadau wanakaa kujadili haya haya ambayo tuna yajadili leo, Mhe. Waziri hawa watakudanganya hapa kama mawaziri wenzako walivyo wahi kudanganywa  huko nyuma alisema Mtaka”, huku akitaka bodi ya Pamba iondoshwe na maafisa wa Bodi hiyo wapangiwe majukumu mengine ambayo wanayaweza, mtaka aliwatupia lawama hizo maafisa hao huku akisema wamekuwa madalali wakuhafanya ubadhilifu wa kuharibu mizani “ Haiwezekani mizani ziharibike halafu aliye haribu asijulikane, Mhe. Waziri hawa wachukuliwe waende maeneo mengine wakasome magazeti ili waje na mawazo mapya”

Mtaka pia amelaani kitendo cha Maafisa wa Bodi ya Pamba kukaa Dar es Salaam, huku matatizo lukuki yakiwa yapo maeneo ambapo pamba inalimwa, ameutaka uongozi huo kuona namna yakuwa karibu na maeneo ambapo Pamba inalimwa kwa wingi badala yakukaa Dar Es Salaam na kungojea kupanda ndege kuja kusuluhisha matatizo.

Katika hatua nyingine, Mtaka alishauri, kama serikali inataka kufanikiwa, zile Milioni 50, ambazo Mhe. Rais aliziahidi kwa kila kijiji wakati wa kampeni ni vema fedha hizo zikaelekezwa kwenye vikundi ili vikundi hivyo viweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo, vinginevyo fedha hizo zinaweza kutafunwa na wajanja wachache ambao watajinufaisha wao na familia zao kama ilivyokuwa kwenye Mabilioni ya JK.

Kwa upande wao chama cha wadau wa Sekta ya Pamba nchini, Tanzania Cotton Association (TCA), wao wameshauri kuondolewa kwa Siasa katika suala la Pamba kwakuwa mipango mingi inakwama kutoka na wanasiasa kuingilia mipango endelevu ya zao la pamba, akisoma taarifa ya chama hicho mwakilishi wake bwana Muhamed Sharifu alisema “ Imefika wakati wanasiasa wakae pembeni na waichie sekta hiyo wadau wafanyekazi yao lakini pia tunawaomba maafisa uagani waache kukaa maofisini na badala yake waende mashambani wakatoe ushauri wa kitaalam” alisema Sharifu.

Hata hivyo kauli hiyo yakuwashutumu wanasiasa ilipingwa vikali na Mbunge wa Geita Vijijini Msukuma Kasheku, ambaye katika kuchangia kwake alidai mtu pekee wakuweza kuyapigania maslahi yamkulima mnyonge ni mwana siasa huku akijinasibu kwakusema hata iwe vipi hawatakuwa tayari kupitisha sheria yakuwaengua wanasiasa kwenye zao la Pamba “Sisi ndio wabunge mtaona kama hilo mnalo litaka litakuwa haiwezekani kila kukicha mnanyonya mkulima halafu leo mnataka eti wanasiasa waondelewe kwenye kulisemea zao la pamba.

Mkutano huo wa siku moja uliandaliwa na Wakala wa Vipimo (WMA) na kuwakutanisha wadau wa sekta ya pamba kutoka mikoa inayo lima Pamba ya Mwanza, Simiyu, Geita, Mara, Shinyanga, Singida, Kigoma, na Kagera kwa minajili yakuangalia vipimo sahihi kwa biashara endelevu ya zao la Pamba.

MWISHO.

 
Axact

Post A Comment: