Nteghenjwa Hosseah, Tamisemi – Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Wilaya
na Wakurugenzi wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ili kutimiza matarajio ya watanzania
ambao wanaitegemea Wizara hii kama chachu ya mabadiliko
katika utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya Tano.
Mhe.Jafo
ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi
wa Halmashauri za Mikoa ya Dar es Salaam, Shinyanga, Mbeya, Songwe, Rukwa,
Ruvuma, Iringa na Njombe yanayoendeshwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa
ushirikiano na Taasisi ya Uongozi.
Akiungumza katika
ufunguzi wa mafunzo hayo Mhe.Jafo amewataka viongozi hao kutumikia
Wananchi kwa kuzingatia Taratibu, Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma huku
wakizingatia mipaka yao ya Utawala, kuboresha mahusiano katika maeneo ya kazi
na kuhakikisha hakuna muingiliano wa
majukumu baina ya viongozi wa Wilaya na Halmashauri.
![]() |
Baadhi
wa wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa
walioshiriki kwenye mafunzo ya uongozi yanayoendeshwa na Ofisi ya Rais Tamisemi
kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi.
|
“Nafahamu baadhi viongozi mlitokea katika sekta binafsi na humkuwa
mnafahamu vizuri utendaji kazi wa shughuli za Serikali hata hivyo mmefanikiwa kwa kipindi chote kutenda kwa kadiri ya
maelekezo ya Serikali,vipaumbele na miongozo mbalimbali iliyotolewa pia mmejitahidi kutoa huduma bora
ukiachilia mbali mapungufu madogo madogo ambayo tumeyabaina na kuyashuhudia
katika baadhi ya maeneo” alisema Jafo.
Aliongeza kuwa “kupitia
mafunzo haya ni imani yangu kuwa wote sasa tutakuwa na uelewa wa pamoja wa
kufanya kazi Kimkakati ili kuwaletea wananchi maendeleo huku mkifahamu vyema
Muundo wa Serikali na namna inavyofanya kazi kwa kuzingatia mipaka na mgawanyo
wa majukumu, Itifaki, utunzaji wa Siri za Serikali na maadili ya viongozi wa
Umma”.
Aidha Mhe. Jafo aliwataka viongozi hao
kuendelea kusimamia nidhamu ya watumishi, kuendeleza mapambano dhidi ya Dawa la
kulevya, kulinda amani na utulivu katika maeneo yao huku wakisimamia kwa makini mapato na matumizi ya
Fedha za Serikali na kusisitiza matumizi ya mifumo ya Kielektroniki katika
ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Akimkaribisha Mgeni
rasmi katika mafunzo hayo Naibu Katibu Tamisemi anayeshughulikia Afya Dkt. Zainabu Chaula amesema kitu cha
msingi kati yetu sisi watendaji ni umoja ambao kupitia huo utatuleta Ushindi na muongozo wa utendaji wetu uko kwenye ilani
ya Chama cha Mapindui hivyo kila mmoja wetu arejee Ilani ile ili afahamu nini
anachotakiwa kukifanya katika kipindi hiki cha miaka mitano.
Awali akitoa
taarifa ya utangulizi kwa mgeni rasmi na
washiriki wa mafunzo hayo Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja alisema mafunzo haya yanatolewa na wataalamu
walioboea katika masuala ya uongozi na yatafanyika kwa muda wa siku tano kwa
viongozi aidi ya 72.
Aliongeza kuwa maeneo
ambayo yatajen gewa uwezo ni namna bora ya kufanya maamuzi ya kimkakati yanayozingatia
mahitaji na manufaa mapana ya Taifa, namna bora ya kuongoza watu na kusimamia Rasilimali
za Taifa na pia jinsi ya kujijengea Sifa za kiungozi ambazo zinaleta
heshima kwa jamii, kuaminika na kutegemwa katika kuleta mabadiliko.
Mafunzo haya yamepangwa
kufanyika katika awamu nne(4) ambapo awamu mbili tayari zimekwsihafanyika
ziliojumuisha Wah. Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kutoka Mikoa kumi na
mbili(12) ya Dodoma, Morogoro, Singida, Tabora, Kigoma, Katavi, Kagera, Mwana,
Mara, Simiyu, Geita na Manyara.
Awamu ya kwanzaya
mafunzo haya ya Uongozi yalifanyika
Mwezi Mei, 2017 na yalifunguliwa na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na awamu ya mwisho inatarajiwa kufanyika
kabla ya mwezi Disemba 2017.
Post A Comment: