·      Kamati ya Bunge yagomea Taarifa.
·        Wapewa saa 15, kuwasilisha mbadala wa Taarifa.

Wataalam wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza na mmoja kutoka TAMISEMI wakiwa wanafatilia kwa karibu mambo yanavyojiri wakati Kamati hiyo ilipokuwa inafafanua sehemu ambazo haikuridhika nazo.


Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza akinukuu baadhi ya mambo.
Na: Atley Kuni- Mwanza.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida hapo jana kamati ya Bunge ya kudumu inayohusika na Wizara ya Tawala za Mikoa na  Serikali za Mitaa (TAMISEMI), iligomea kuipokea taarifa ya fedha na Miradi ya halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa madai kwamba fedha ambazo zilipaswa kupelekwa kwenye miradi ya wananchi
Hapa Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Ndaro Kwilijira (kulia) akiwa ananukuu mambo yanayo jitokeza, kutoka kushoto ni Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Minja na katikati ni Diwani wa  Igoma Mhe. Chagulani. wakati wa kikao hicho.
zilitumika ndivyo sivyo.
Akisoma kwa niaba ya kamati Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Hamis Kigwangala alisema fedha ambazo zilipaswa kupelekwa kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi zimetumika kwa ajili ya shughuli za kiutawala na sio  miradi iliyokusudiwa, huku akihoji kutokuwepo na mchanganua wa fedha hizo na jinsi zilivyo ingia na kwenda kwenye matumizi. “ kwa hiyo hata fedha ndogo iliyokuja kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shule ya msingi Lwamnyima, ambao ulikuwa unahitaji shilingi milioni 31 kwa ajili ya nyumba za walimu hazikupelekwa na badala yake zikawekwa kwenye shughuli za Administration” anasema na kuongeza “hivyo wajumbe wa kamati wanahoji uchungu wa nyie watumishi wa jiji katika kuwaletea wananchi maendeleo”.
Kipengele kingine kilicho zua utata ni cha kuandaa mpango mkakati wa jiji la Mwanza, ambapo wajumbe walisema fedha iliyokuwa imepangwa kwa ajili ya shughuli hiyo ilipokelewa na ikatumika lakini cha ajabu matumizi ya  fedha hiyo nayo ilielekezwa  kufanya shughuli za kiutala.
Mabali ya matuymizi hayo kamati hiyo pia ilihoji juu ya fedha za mgao katika ngazi za Kata kuwa, kwa mujibu wa taratibu za fedha ugawaji wa fedha kwenye kata hufanyika kwa kuzingatia vigezo ambavyo halmashauri husika imejiwekea, na suala la  idadi ya watu ikitajwa kama kigezo muhimu katika ugawaji wa fedha, kinyume na jiji la Mwanza ambao wao wamekuwa wakigawa fedha kwa uwiano ulio sawia bila kuzingatia idadi ya watu, hivyo kamati hiyo ikaomba ufafanuzi wa vigezo vilivyo tumika kugawa, milioni tano tano kwa kila wilaya bila kujali ukubwa wa kata na Idadi ya watu waliopo kwenye kata husika.
Kama hiyo haitoshi kamati hiyo ya Bunge ilienda mabali zaidi na  kuhoji juu ya makadirio madogo ya makusanyo ya ndani na jinsi fedha hizo zinavyo ishia mikononi mwa watu wachache bila kuwapelekea wananchi maendeleo, huku akitolea mfano mwaka uliopita kwamba, Halmashauri ya Jiji la Mwanza ilipanga katika bajeti yake kukusanya Bil. 2.6 katika mwaka wa 2012/ 2023 lakini katika jambo la kushangaza ikakusanya kiasi cha Mil. 494 tu ambayo alisema ni asilimia ndogo sana kama 20% tu. “hakuna walakini,? Alihoji Kigwangala… “Tunafahamu watumishi wa halmashauri mnakula sana fedha za (Own source), na mnafanyaje nikwa ku fluctuate makusanyo ya ndani” alisema kwa msisitizo.

Mwishoni Mwenyekiti huyo wa kamati, alimuomba Mhe.Wilaya ya Ilemela, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana pamoja na Mhe. Mkuu wa Mkoa Mwanza kukutana na kamati hiyo ili kujua mgongano wa kiutawala uliopo baina ya Halmashauri Jiji na Ilemela, kwakuwa suala la mgawanyo wa mali baina ya Halmashauri ya Jiji na Ilemela havikuwa sawa na kwamba kuna hoja zilizo ibuka kutoka Ilemela juu ya uwiano usio sahihi, “ile instrument wakati mnagawana mali ilikuwa ina eleza wazi juu ya zitakazo kuwa mali za Ilemela na zile zitakazokuwa za Jiji, lakini kwa malalamiko tunayo yapata kutoka Ilemela kwamba baadhi ya miradi iliyopaswa kuwa Ilemela bado ipo Jiji”, anasema Kingwangala na kuongeza “hata kama ikiwezekana tubadilishe
 
structure ya kiutawala”

Akihitimisha mwenyekiti huyo alisema, kwa maana hiyo wao kama wajumbe wa kamati wamepitia na hawajaridhishwa na kwa mantiki hiyo wakatoa muda usiozidi saa 15 ili wapatiwe majibu ndipo waweze kuendelea na shughuli zao katika Wilaya zingine.
 
Kamati hiyo ipo Mkoani mwanza kwa ajili ya kupitia shughuli mbali mbali za maendeleo na kuona jinsi wananchi wanavyo hudumiwa katika kutekeleza suala la utawala bora wa watu.
Awali Nyakati za asubuhi siku ya jana Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi  Evarist Ndikilo, aliwapokea na kuwapa taarifa fupi kuhusu hali ya Mkoa na shughuli zinazofanyika mkoani hapa ikiwa ni pamoja na jitihada zilizopo katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Mwanza.


 
Axact

Post A Comment: