SIDO Mwanza
Maonesho ya Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO)  yanayo fanyika jiji Mwanza katika Viwanja vya Nyamagana, yameonekana kuwa kivutia kikubwa kwa wakaazi wa Jiji hilo, Mwandishi wa Blog hii alivyofika alishuhudia bidhaa mbalimbali zilizo tengenezwa na Wazalendo wa nchi hii zikwa zimepedeza, nakufanya kununuliwa na wadau Mbalimbali waliofika kujionea Maonesho hayo.

Katika siku za hivi karibuni Mkoa wa Mwanza umeendelea kuwa kivutio kikubwa hasa katika suala la Uwekezaji kwani Mkoa huo Unatajwa kukuwa kwa kasi kubwa Miongoni mwa Miji iliyoko kusini Mwa Jangwa la Sahara.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa huo Evarist Ndikilo, Mapema wiki hii akifungua Mkutano wa Kutathmini Malengo ya Millenia kwenye Hotel ya Gold Crest alisema Amani ni suala muhimu sana katika kujiletea Maendeleo, hivyo akawaasa wana Mwanza na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanailinda hali ya utulivu iliyopo, kwana itasaidia wana Mwanza kujiletea Mandeleo kwakufanya shughuli zao bila yakuwa na wasiwasi.
Na Atley Kuni Mwanza.
Next
Newer Post
Previous
This is the last post.
Axact

Post A Comment: