Kikao cha uwekezaji kanda ya Ziwa kinafanyika hii leo katika Ukumbi wa halmashauri ya Jiji, kwa mujibu wa ratiba ambayo Mtandao huu imezipata ni kwamba mkutano huo unakuja mwezi mmoja baada ya kuhahirishwa kwa kongamano hilo.

Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Uwekezaji tayari kwa kikao.
Kongamano la Uwekezaji kanda ya ziwa  linalo jumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Kagera na Mara linakusudi la kuelezea hali ya Uwekezaji katika kanda ya ziwa na fursa zilizopo katika kanda hiyo.

Hata hivyo Kongamano hilo lilikuwa  limepangwa kufanyika kati ya Novemba 14 hadi 16, 2013 sasa lime ahirishwa hadi Februari 2014 na kwa mujibu wa tangazo lao tarehe rasmi ya Kongamano hilo ambalo Mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano itatangazwa hapo badae.
Axact

Post A Comment: