.NA  FRANCIS GODWIN -- IRINGA
Tanzania yazibagwa nchi sita barani Afrika katika mashindano ya vyuo  vikuu ya  kuwania tuzo ya heshima   ya sheria  za  vita  yaliyomalizika  hivi karibuni .


Katika  shindano hilo lililofanyika   kati ya Novemba   16-23 mwaka  huu  jijini  Arusha chuo  kikuu  cha Iringa  kiliwakilishwa na  washiriki  watatu  ambao ni Anneny Nahum ,Janeth Nagai   na Joanna Mcintype vijana  hao  waliweza kufanya  vema  kiasi  cha  kuiwezesha nchi ya Tanzania kuibuka mshindi  wa kwanza wa  tuzo hiyo.

Wakizungumza leo chuoni  hapo katika hafla  fupi ya kukabidhi  tuzo hiyo kwa uongozi wa  chuo hicho ,washirikia hao  walisema  kuwa  ushindi  huo  umetokana na ushirikiano  ulioonyeshwa na nidham iliyotukuka miongoni mwao.

Hata  hivyo  walisema  kuwa  tuzo  hiyo  ni  heshima kubwa kwa Tanzania  na ni heshima kwa  chuo  hicho .

mkuu msaidizi wa  kitivo cha  sheria chuo kikuu cha Iringa Jane  Massey alisema  kuwa washiriki hao  wamepata kushinda kutokana na kuonyesha  uwezo wa hali ya  juu katika mashindano hayo na  kuwa  heshima kubwa ambayo  chuo hicho  imepata  ni jambo na kujivunia na kumshukuru Mungu  pia. Alisema  kinachoangaliwa katika mashindano hayo na lengo la tuzo hiyo ni kuenzi amani na kuona hakuna matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu ambayo yanatokea wakati wa vita ,hivyo sheria  hiyo  inapaswa  kuendelea  kutolewa hata kwa Tanzania pia

Kwa  upande wake makamu Mkuu  wa  chuo   kikuu  cha Tumaini Iringa, Prof Nicholaus Bangu alisema  kuwa chuo  hicho  kitaendelea  kufanya  vema si katika mashindano pekee  bali katika mambo mbali mbali yakiwemo ya  kitaalum .

Kwani  alisema  kuwa moja kati  ya mambo  yanayozingatiwa katika  ufundishaji chuoni hapo ni pamoja na kuwafundisha  wanafunzi katika maadili na nidham na ndio mafanikio ya wanafunzi kufanya vema.

Tuzo  hiyo  ambayo  inatolewa kama  njia ya kumuenzi aliyekuwa mwanzilishi wa msalaba mwekundi  ilianzishwa  mwaka 2010 na  kuanza  kushindaniwa  mwaka 2011 ambapo ilichukuliwa na nchi  ya  Ephiopia  ilinyakuwa kwa mara ya kwanza na mwaka 2012 ilichukuliwa na Kenya na  mwaka huu Tanzania i meweza  kuzishinda nchi   hizo sita  ambazo ni South Afrika, Uganda,Kenya, Rwanda, Ethiopia na Zimbabwe

 
Axact

Post A Comment: