Tumeshuhudia   jamii   ikikumbwa  na
ukatili  wa  kijinsia   hasa
kwenye  vipigo, lakini  kwa
msichana  Juliana  mambo yalikuwa ni  tofauti  yeye  ni  mtu   aliyeonja  ukatili
wa
kijinsia  katika  Nyanja  ya  kielimu.
Baba mzazi wa Juliana aliamua makusudi kuelekeza ukatili wa
kijinsia  kielimu kwa binti yake,
fuatilia  makala  hii  yenye  simanzi  na
masikitiko.
Baba   hakutaka nisome  kabisa, kwani
kila mara  nilipomwambia kuwa nahitaji  kusoma
aliniambia  kuwa, kusoma kwa mtoto wa
kike  hakuna  maana  yoyote mtoto wa
kike  ana jukumu moja  tu, ambalo nikuolewa. Alisema
Juliana alipokuwa akinisimulia  kisa  chake huku
akitokwa na machozi.
Juliana  aliniambia kuwa  kila  mara  alijitahidi  kumshawishi
Baba  yake  juu  ya  yeye  kupelekwa   shule  lakini  Baba yake    alilirudia  kauli  yake  kuwa,
kusoma ni wajibu wa mtoto wa kiume. Baba  yake
Juliana  alikuwa na watoto  wane, watatu  wakiwa
wanaume, kwa upande wa  watoto wa kiume wote walipelekwa
shule  kasoro
ni  Juliana  tu  ambaye alinyima  haki
ya  kielemu.
Ni
ukweli  usiopingika  kuwa  kunyimwa   kwa
fursa  kwa Juliana  kulimfanya
Juliana  awepo  hapo nilipomkuta, nilikutana  na
Juliana katika  standi kuu  ya  mabasi  ya
Nyegezi   Jijini Mwanza akiwa  ameketi  kwa
hudhuni huku pembeni yake  kukiwa na sufulia  la uji
wa ulezi aliokuwa akiuuza.
Kutokana na kuwa mapema  sana  asubuhi
wateja  walikuwa  hawajafika  eneo  hilo,
hivyo basi nilipata  nafasi  ya kumuuliza juu
ya  maisha yake   yaliyomfanya ajikute kuwa mama
lishe  au ntilie , hapo ndipo aliporejea  historia  yake
ya miaka  kumi  iliyopita
iliyojaa  uchungu  na masikitiko  ya ukatili wa
kijinsia  katika  Nyanja  ya  elimu.
 Juliana alisema kuwa  kaka  yangu namini
leo  hii  na mimi ningekuwa
kama  mama  Anne Makinda ambaye ni spika wa Bunge la Jamhuri  ya
Muungano wa
Tanznaia,  endapokuwa  baba  yangu  hasingenitendea  unyama  wa
kijinsia kwa kuninyima  haki  ya kuwa na
elimu  basi  ningekuwa
mbali  kaka  yangu,
lakini  ndiyo  hivyo  tena
naishia  kwenye kuuza uji.
Juliana    aliniambia  kuwa,   kaka
yangu   makubwa
yalinipata  kwani  nakumbuka  mara  kwa mara 
nilikuwa  namkumbusha 
baba  juu  ya  kiu  yangu  ya  kusoma,
lakini  kuna siku  sitaisahau, kwani  nilipomkumbusha  baba  juu 
ya  suala hilo, aliishia  kunipiga  huku  akiniambia 
nishike  kichwa  changu kwa mikono  miwili  na
kumzunguka  alipokuwa  amesimama  bila  idadi  ya mzunguko.
Ikumbukwe kuwa  katiba  ya  jamhuri  ya
muungano wa Tanzania  ibara  ya  13: 6 inasema
ni marufuku   kwa mtu  kuteswa, kuadhibiwa   kinyama  au kupewa  adhabu  au
kumdhalilisha. Mimi  naamini  kama mwandishi  natumia  nafasi  hii  kupinga 
ukatili   wa kijinsia  hasa kwa kutumia  mbinu 
za   za kuripoti  
ukatili  wa
kijinsia   kama  TAMWA walivyoamua  kuwajengea 
uwezo  waandishi wa habari  kuripoti  matukio  hayo.
Chama  cha 
wanahabari  wanawake  Tanzania  (TAMWA) 
kimekuwa  kikipiga  kelele    huu  ya 
ukatili wa kijinsia , lakini  bado  kuna maeneo jamii    inaendelea 
na vitendo  hivyo.  Ni
wazi  kuna   Msichana 
Juliana  alinyimwa  haki  yake  ya kusoma kwa kuwa 
tu  yeye  ni  msichana, huo  ni
ukatili  mkubwa wa
kijinsia. 
Kwa sasa  Juliana  anaendelea  na
biashara  yake 
ya  mamaNtilie  na  amejiwekea  malengo  ya 
kukusanya  fedha  kidogo kidogo  na mwakani  ana  mpango wa kuanza 
kujiendeleaza  kielimu  kwa kupitia elimu  ya watu  wazima.
 
 
Post A Comment: