Chama  Cha  wandishi wa habari  wanawake  Tanzania (TAMWA) kimeendelea na juhudi  zake  za kuwafunda  waandishi wa habari  mbinu  za kuripoti  na  kuandika  habari  za ukatili wa kijinsia   ili kumaliza  tatizo  hilo  linaloonekana kuwa sugu  katika jamii
Waandishi    zaidi  ya  ishirini  toka mikoa  ya  kanda  ya  kanda  ya ziwa ikijumuisha Mwanza, Shinyanga, Bukoba  na Kagera  wamenufaika  na mafunzo  hayo  kwa kupata miongozo  ya  jinsi  ya  kuandika  habari za  ukatili wa kijinsia.
Mwezeshaji  mkongwe wa mafunzo hayo  Bwana Ndimala  aliwafunza washiriki wa mafunzo  hayo  jinsi  ya  kutumia vipaji  vyao  kuisaidia jamii  iondokane  na  ukatili wa kijinsia.
Naye  mshiriki wa mafunzo Bwana  Revocatus  Herman  amesema  kwamba, mafunzo  hayo  yatamsaidia  kwa kiasi kikubwa  kufahamu namna  bora ya  kuandika habari za kijinsia  ili  kuleta  mabadiliko  katika  jamii  juu  ya  utatili wa kijinsia.
TAMWA  wamekuwa na programu  endelevu  ya  kutoa  mafunzo  kwa waandishi  ili kuwajengea  uwezo katika  kazi  zao. Mafunzo  hayo ni  awamu ya  pili kwa mwaka huu kufanyika .
TAMWA  inawasaidia waandishi  kufahamu mambo  mbalimbali kama wajibu wa watunga  sera kutika kukabiliana  na ukatili wa kijinsia, mkataba wa SADC kuhusu jinsia na  maendeleo  na  aina  za ukatili wa kijinsia.
 
 
Awali  yalifanyika kwa   siku nne  na awamu ya pili  yalifanyika kwa siku mbili  katika    hotel  ya midland Jijini Mwanza.
 
 
 
 
Imeandaliwa na   Na: Neema Joseph,   Mwanza
 
Axact

Post A Comment: