Nina  wapongeza wananchi  waliojitokeza na kujenga Nyumba bora katika Vijiji hivi vya Nyampanda, Isole na Luchili Wilaya ya Sengerema, lakini pia niwa ahidi kushirikiana nanyi katika kupata unafuu wa vifaa vya Ujenzi ili muweze kuwa na nyumba bora.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo wakati akikabidhi mabati miamoja na ishirini tatu kwa wananchi wa Wilaya ya Sengerema kwenye Vijiji vya Isole, Nyampande na Luchili yaliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya hiyo kama sehemu ya kuboresha maisha ya wananchi wa maeneo hayo, ikiwa ni mkakati wa halamashauri hiyo kutenga bajeti ya Mil.15 kila mwaka kwenye vyanzo vyake vya ndani.

Ndikilo alisema ilikuwaboreshea maisha wananchi serikali ya Mkoa haitasita kuwasiliana na Mheshi,iwa waziri mkuu na wenye viwanda ili wananchi watakaoweza kujenga maboma waweze kupatiwa mabati kwa bei nafuu ya kiwandaani “ Kama serikali ya Mkoa tutaona namna nzuri ya kuwasiliana na Mheshimiwa waziri mkuu ili tuweze kuwasaidia wananchi waondokane na makaazi duni” alisema na kuongeza kuwa “hizi jitihada zinazofanywa na halmashauri nizakupongezwa kwakuwa hata nchi ya Korea kusini ambapo viongozi wenu walikokwenda kujifunza nao walikuwa kwenye umaskini miaka mingi iliyopita lakini kubuniwa kwa mkakati kama huu ndio maana wanachi hao walifanikiwa kuboresha maisha yao.

Adha Ndikilo aliongeza kuwa lengo la mikakati kama hiyo ambayo imebuniwa na Halmashauri ya Sengerema ni mfano wa kuigwa kwa halmashauri zingine za Mkoa wa Mwanza, “ Ndugu zangu mpango huu ambao Wilaya ya Sengerema imeamua kuufanya ni dhahiri kwamba hii ni dhamira ya dhati katika kuwaletea wananchi maendeleo”.

Aidha alisema endepo kama kuna watu ambao ni akina Tomaso kwao kuamini hadi waguse makovu na Vidonda vya Yesu sasa waje waone jinsi ninyi mlivyonufaika na mpango huu, maana inasemekana wengine walipokuwa wanaambiwa unajenga nyumba na serikali inakupatia mabati walikuwa wanadhani ni mzaha sasa leo waje wajionee hapa kwenu “ Serikali hii ni sikivu iki ahidi inatimiza, alisema mkuu huyo wa Mkoa na kuongeza kuwa mradi huo kwamba sio wa kilaghai wananchi wakijiunga na kufyatua matofali wakajenga Halmashauri itawapatia mabati.

Awali kabla ya hotuba ya mkuu wa Mkoa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, alisema Mradi wa Saemaul Undong ulianzishwa wilayani humo mwaka 2009, ukiwa na vijiji vitatu vya mfano vya Isole Nyampande na Luchili, kufatia maarifa yaliyopatikana kutokana na wajumbe Mathew Lubongeja na Ndg Silas B Ntego waliotembela nchini Korea Kusini kujifunza kwa jinsi wananchi wanavyo ungana katika kuchuochea  shughuli mbali mbali za maendeleo na hapo awali ulijikita kwa kaya ambazo ni masikini sana katika suala la makaazi duni.

Alieleza kwamba tayari mradi huo ulikwisha nunua mabati 920 na kuyagawa kwa kaya 20 na kuyagawa kwa wanachi wa kijiji cha Isole na bade mabati 123 yaliyo gawiwa na Mkuu wa Mkoa kwenye kaya 3 na hivi sasa wannchi wengine wanaendelea na ujenzi.

Kwa upande wao wananchi walio nufaika na mradi huo walisema wanaipongeza Serikali kwa kuwajali na kuwa na mipango inayo tekelezeka, Msagwa Kafula ambaye alikuwa mmoja wa wanufaika wa mpango huo alisema “ Kama serikali ina ahidi na kutekeleza unadhani sisi tufanyeje siku ishukuru,…, Mhhh.., kuwa kiongozi ni pamoja na kuwa mbunifu na uthubutu” alisema na kuongeza kama hawa madiwani wasingethubutu kwenda Korea unadhani wangetoa wapi huu ujuzi? Naye Nestori Malimbita alisema “ nadhni na wale wengine waliokuwa hawaamini sasa watajua kwamba ni kweli.

Hata hivyo pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto zinazo jitokeza katika kutekeleza mpango huo wa makaazi bora ikiwapo mwamko mdogo kwa wananchi pamoja na upatikanaji wa rasilimali fedha na mbao, jambo ambali Ndikilo aliahidi kulipaatia ufumbuzi

Mkuu huyo wa mkoa alikuwepo Wilayani humo kwa ziara ya kikazi kwa kukagua shughuli za maendeleo, kuzungumza na wanachi na kusikia kero zao lakini pia kufanya Mikutano ya hadhara kuelezea Mipango iliyopo ya Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo yao.
Axact

Post A Comment: