Watu wasio fahamika kwa idadi wamefukiwa katika Machimbo ya Moramu ya Terati yaliopo Mkoani Arusha.

HAYA NI MOJA YA MACHIMBO YA MORAM YANAYOPATIKANA MKOANI ARUSHA( Picha na Maktaba).
Taarifa hiyo imeujulisha Mtandao huu kuwa, machimbo hayo ambayo yapo nje kidogo ya mji wa Arusha yalisha pigwa marufuku na Mkuu wa Mkoa huo Bwana Magesa Mulongo.

Hata hivyo hadi habari hii inakwenda mitamboni, tayari watu wawili walikuwa wameopolewa na wengine kadhaa ambao idadi yao haijafahamika bado wamenaswa chini ya kifusi hicho.

Habari hiyo imeongeza kwamba tayari Jeshi la Zima moto, Jeshi la Polisi na wananchi mkoani Arusha wamefika eneo la tukio na wanaendelea na shughuli za uokoaji hata hivyo imeelezwa kuwa bado miundombinu ya Uookoaji ni duni kwani vifaa kama Beleshi na Majembe ndio vinavyotumika katika ukoaji huo.

Kamanda wa Polisi Mkoani humo Leberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Axact

Post A Comment: