Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto hatakiwi kuwepo wakati wote wa kesi yake ya uhalifu dhidi ya ubinadamu huko The Hague, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) iliamua Jumatano (tarehe 15 Januari).

"Baraza limemruhusu kwa masharti Bw. Ruto kutokuwepo wakati wote katika kesi, "jaji wa ICC Chile Eboe-Osuji alisema.

Mahakama iliamua mwezi Oktoba kwamba ikibadili uamuzi wa awali wa kumsamehe katika kesi zake nyingi.

Uamuzi wa mahakama wa hivi karibuni unaeleza kwamba Ruto lazima awepo katika usomwaji wote wa uamuzi, kama inawezekana, hukumu.

Pia lazima awepo "wakati waathirika wanatoa maoni yao na wasiwasi binafsi" na kwa siku tano za kwanza za kusikilizwa kufuatia kipindi cha mapumziko.
Axact

Post A Comment: