Vinathamani ya Mil. 10.
 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo amekabidhi vifaa vya hasptali vyenye thamani ya Tsh.Mil. 10 kwenye Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana vilivyotolewa na Benki ya Dimond katika harakati zake za kuiwezesha jamii kuwa na huduma bora za afya.
 
Amewasa watendaji wa Hospitali hiyo kuvitunza na kuhakikisha vinadumu ili kuiwezesha jamii ya Wilaya hiyo kupata huduma bora za afya, akikabidhi vifaa hivyo Ndikilo amesema, Hospitali pekee inayo tegemewa kwa hivi sasa ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekouture ambayo kwa siku za hivi karibuni imeoneka kuelemewa kutokana na kukuwa kwa mji lakini pia kutegemewa na Mikoa ya Jirani.
 
Amesema Benki ya DTB imeonesha mfano hivyo kama wadau tunayo kila sababu ya kuwaunga mkono kwa kufungua akaunti katika benki hiyo kwani kwa kufanya hivyo itawapa moyo DTB na kuwawezesha kuendelea kutoa huduma pindi watakapo hitajika.
 
Naye Mwakilishi wa DTB Tanzania Bw. Sylvester Bahati, amesema wao kama DTB walicho kitoa sio msaada bali ni huduma kama huduma nyingine ambayo ingeweza kutolewa na mdau mwingine yeyote. "Sisi hatupendi kuita msada kwakuwa hii ni sehemu ya faida kwa jamii ambayo kama DTB huwa tunatoa kila mwisho wa mwaka" alisema na kuongeza kwa kutolewa kwa vifaa hivyo ni kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya DTB na halmashauri ya Jiji la Mwanza.
 
Kwa upande wake mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza alisema, kama Mstahiki meya anayetokana na chama Tawala ni kuhakikisha ilani ya Chama cha mapinduzi inatekelezwa kwa vitendo kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya kuingoza serikali tangu walipo nadi Ilani ya chama hicho 2010 na kufanikiwa kushika dola. " Ndugu zangu wana Nyamagana na wana Mwanza kwa ujumla kinachotendeka hapa ni kuhakikisha ilani ya CCM inatekelezwa kwa vitendo na sio kelele za majukaani ambazo hazimsaidii Mwananchi wa kawaida. 
 
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Butimba Mhe. Dismas Masumu, ameipongeza Benki ya DTB kwa mpango wake wa kuwa bega kwa bega na wanachi katika kuimarisha huduma mbali mbali za kijamii.
 
Vifaa vilivyotolewa ni Trolley-Dressing/ Dispensing Screen, Delivery kit, Kidney dish, Diagnostic set (Retinoscope), Bed sheet, Wheel Chair Sunction Machine, Mosquto Nets na Gumboot.
 
Hii ni mara ya kwanza kwa benki hiyo kutoa huduma ya vifaa ya Hospitali kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ;lakini imekuwa ikitoa huduma mbali mbali katika Wilaya zingine hapa nchini.
Axact

Post A Comment: