Na: Bosire Boniface, Garissa

Maofisa wa Kenya wamepuuza Ripoti ya Dunia ya hivi karibuni kabisa ya kila mwaka ya shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch (HRW), ambayo ilitoa tathmini ya ukosoaji uliyo mkali kabisa kuhusu maendeleo na kinga ya haki za binadamu nchini Kenya kwa mwaka uliopita,

Hatua ya taratibu ya mabadiliko ya polisi nchini Kenya, utamaduni wa kutoadhibiwa kwa unyanyasaji unaofanywa na vikosi vya usalama na serikali kushindwa kuwawajibisha wakosoaji wa vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007-2008 kumebakia kuwa kero kubwa, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Miongoni mwa mambo mengine, ripoti hiyo ilihoji kiwango cha ushirikiano wa serikali na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) katika uhalifu dhidi ya ubinadamu wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Makamu wa Rais William Ruto.

"Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta na makamu wake, William Ruto, imekuwa ikitumia ushindi wake mdogo wa kura asilimia 50.7 ikikwepa duru ya pili ya uchaguzi kusambaza rasilimali zote za nchi katika kusimamisha mashtaka yao kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu wa Kivita kwa majukumu yao ya uongozi yanayodaiwa katika vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007-08," ripoti hiyo inasema.

"Kenya iliapa kuendeleza ushirikiano na ICC, lakini kutoka uchaguzi, serikali mpya imepiga kampeni kubwa katika Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kufutwa kwa mashtaka yao, kuahirishwa au kupelekwa katika njia za sheria za ndani," inasema.

Katika kujibu, Waziri wa Mambo ya Nje Amina Mohamed aliitaja ripoti ya HRW kuwa "ya kukasirisha na isiyoeleweka".

"Kwamba nchi haishirikiani na ICC siyo kweli kabisa," aliiambia Sabahi. "Mahudhurio ya Makamu wa Rais Ruto katika mahakama wakati anapohitajika ni ushahidi kwamba kuna ushirikiano. Rais Kenyatta hajasema kwamba hatahudhuria kesi yake wakati itakapofikia kusikilizwa mwezi Februari."

Bado mashtaka ya Kenyatta, ambayo yamepangiwa kuanza tarehe 5, Februari, yameairishwa bila kuja siku ya kuendelea baada ya Mwendesha mashtaka mkuu Fatou Bensouda kutaka muda zaidi kukusanya ushahidi na utetezi kuomba kusimamisha mashtaka.

"Kesi za ICC nchini Kenya zimekuwa zikizuiwa na kujitoa kwa mashahidi wa mashtaka, ikituhumiwa kwa sababu ya rushwa na vitisho; walalamikiwa pia wametuhumu kuharibiwa kwa ushahidi au vitisho kwa mashahidi," ripoti hiyo ilisema, ikiongeza kwamba mwendesha mashtaka wa ICC alikiita kiwango cha kuwachezea mashahidi katika kesi kuwa "hakijawahi kutokea".

Kwa kampeni ya Kenya kujitoa katika ICC  na kuziomba nchi nyingine za Umoja wa Afrika kufanya hivyo, Mohamed alisema kulifanyika ndani ya muundo wa sheria za ndani na za kimataifa.

Kenya inafuata taratibu zote zinazofaa katika hatua hiyo "kwa uwazi na sio kwa siri," Mohamed alisema. "Waandishi wa ripoti hiyo wana ajenda ya siri lakini tutaendelea na uhusiano unaojenga na ICC."

Polisi wa Kenya watuhumiwa

Polisi pia ilipuuza matokeo ya ripoti ambayo ilituhumu vikosi vya usalama kwa mauwaji ya bila kushtakiwa, mateso na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu.

"Utafiti uliofanywa na Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya uligundua kwamba polisi waliwaua kinyume cha sheria watu 120 kati ya Mei na Agosti 2013 katika hali ambayo ingeweza kuzuilika, na kwamba polisi haikuripoti mauaji hayo kwa mamlaka ya kiraia inayoisimamia, Mamlaka Huru ya Usimamizi ya Polisi, kwa ajili ya uchunguzi kama inavyotakiwa chini ya sheria," ripoti ilisema.

Ripoti hiyo pia iliitaja polisi kwa "mateso, upoteaji, na mauaji kinyume cha sheria ya wanaotuhumiwa kwa ugaidi na watu wa asili ya Kisomali".

Inspekta Jenerali wa Polisi wa Kenya David Kimaiyo aliiambia Sabahi madai katika ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu ilizingatia mwenendo wa vikosi vya usalama miaka mingi iliyopita, ikiongeza kwamba katika miaka ya hivi karibuni, maofisa wa usalama wamekuwa waathirika wa magenge ya wahalifu na makundi ya magaidi ambayo ripoti imekwepa makusudi kutaja.

"Nchi inakabiliwa na vitisho vya vurugu kutoka pande zote," alisema. "Katika matukio kadhaa maofisa usalama imebidi wachukue hatua kwa kujizuia na pale ilipolazimu kutumia nguvu. Baadhi ya wahalifu hawawezi kutendewa kwa upole."

Katika kujibu tuhuma za ripoti ambazo wanaharakati wa chama cha kiraia wako katika shinikizo la kuacha kutetea haki kwa waathirika wa vurugu za baada ya uchaguzi, Kimaiyo alisema kwamba polisi ingeweza kutoa ulinzi kwa Wakenya wote, ikiwa ni pamoja na wanaharakati wa vyama vya kiraia na familia zao.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Idara ya Polisi Johnstone Kavuludi alikiri kwamba mchakato wa marekebisho ya idara ya polisi ulikuwa unachelewa, lakini alisema tahadhari ilikuwa lazima.

"Ni kweli kwamba marekebisho yako nyuma kiasi, lakini sasa tunajipanga na kufanya kazi ya kuharakisha marekebisho," aliiambia Sabahi. "Mchakato unaweza kwenda taratibu, lakini pia tunataka kuendesha uchunguzi wa haki kwa wale wote ambao uadilifu wao na rekodi ya haki za binadam vimetiliwa mashaka”

Uhuru wa vyombo vya habari wahojiwa

Kwa upande wake, Waziri wa Habari Habari, Mawasiliano na Teknolojia Fred Matiang'i alikanusha tuhuma za ripoti hiyo kwamba serikali ilikuwa ikizuia uhuru wa vyombo vya habari kwa kuanzisha  “ zuio kali kuhusu vyombo vya habari na mashirika yasiyo na ingiza  faida Alisema kusudi la serikali lilikuwa sio kuvizuia vyombo vya habari. "Sheria ambazo serikali imeanzisha zinamaanisha kuimarisha utoaji wa ripoti sahihi na kuzuia uovu," aliiambia Sabahi.

"Baadhi ya mashirika ya habari yanapotosha kile ambacho sheria mpya zinaeleza kuulaghai umma, na ninashangazwa na mashirika yenye [hadhi] ya Human Rights Watch yameleta uongo kwamba serikali inajikita katika kuzuia vyombo vya habari," alisema.

Hata hivyo, wawakilishi kutoka katika vyombo vya habari na makundi ya jumuiya za kiraia wameiunga mkono ripoti hiyo ya HRW, wakisema inaonyesha ukweli wa hali nchini Kenya.

Makamu Mwenyekiti wa Editors Guild ya Kenya David Ohito aliiambia Sabahi kwamba idhini ya Kenyatta ya sheria mpya kwa vyombo vya habari inatishia kikamilifu uhuru na uhai wa vyombo vya habari nchini.

"Ripoti ya Human Rights Watch iliandaliwa [kabla] sheria hizi hazijatungwa, lakini serikali imetimiza tishio lake na kusaini sheria na kudhibiti vyombo vya habari kabisa," alisema Ohito, ambaye ni mhariri wa gazeti la The Standard.

Alisema wadau wa vyombo vya habari wamekwenda mahakamani kupinga sheria  Marekebisho ya Habari na mawasiliano ya Kenya ya mwaka 2013 na Sheria ya Baraza la Vyombo vya Habari Kenya. Kama sheria hizi hazitapitiwa tena, vyombo vya habari vitakabiliwa na ukaguzi na adhabu kali kutoka serikalini, alisema.

Mwandishi wa habari za picha na mwanaharakati Boniface Mwangi alisema rekodi ya Kenya kuhusu haki za binadamu, nidhamu ya utawala wa sheria na kupambana na rushwa ni mbaya.

"Kutoadhibiwa kumekuwa ni kawaida. Msukumo wa serikali ya Kenya kuondolewa kwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya rais na makamu wake ni picha mbaya kwa wengine, hususan kwa vikosi vya usalama," aliiambia Sabahi.

Rais ana nafasi ya kujisafisha yeye mwenyewe katika mahakama ya sheria na anapaswa kuwadhibiti viongozi wa serikali wanaotoa msukumo dhidi ya kesi ya ICC, alisema Mwangi.

"Kenya iko katika hatari ya kujiunga na nchi ambazo hazina uvumilivu katika uhakiki na uwiano," alisema. "Ndiyo sababu sheria mpya zimeharakishwa kutungwa kuzuia uhuru."

 
Axact

Post A Comment: