.Wananchi wasema Ahadi ya kupiga picha tarehe 25/12/2013. haikuwa kwa Vitendo.
Mhe Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli, alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mwanza siku ya tarehe 14.11.2013, Jijini Mwanza alipofika kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika daraja la Mabatini. Hapa ndipo alipo ahidi daraja kukamilika na kuanza kutumika kabla ya Sikukuu ya Chrismas na Mwaka Mpya wa 2014."Nataka tarehe 25.12.2013, ndugu zangu Wasukuma waliokuwa wanapiga picha kwenye samaki waje wapiga hapa mabatini" 

 
Hapa tuna Sikiliza Ahadi ya tarehe 25.12.2013.
Wanachi katika Mkoa wa Mwanza na hususan wale wanaoishi katika katika ya mji wa Mwanza wamesema, Ahadi aliyoitoa Mhe. Magufuli wakati wa kuweka jiwe la msingi katika daraja la Waenda kwa Miguu la Mabatini lililoko Mkoani hapa haikuwa ya kweli kwani mda umepita hata ule ambao waliahidiwa kuwa daraja lingekuwa tayari.
Tulipiga na Picha ya Pamoja.
 
"Fikiria bwana Kuninews, sisi tuliahidiwa na Mhe. magufuli kwamba tarehe 25.12.Mwaka jana tungepiga picha kwenye daraja hili lakini haijawa hivyo, tafsiri ni kwamba Mheshimiwa waziri kapuuzwa" aliniambia bwana Mashauri Kitambo mkaazi wa Miembe giza Mabatini jiji hapa.
 
Kikundi cha Mchele Mchele kikitumbuiza.
Naye Mariam Mayengela anasema" kama utakumbuka ndugu mwandishi sisi hapa mabatini imekuwa kero ya mda mrefu, matumaini yetu ni daraja likamilike na hili tuta linalo sababisha msongamano liweze kuondoshwa." anasema na kuongeza Nyakati za jioni wewe mwenyewe huwa unaona wananchi tunavyo pata shida, na ... na...!!  tulivyosikia kauli ya Mhe. waziri sikuile tulidhani sasa ukombozi umetimia ndio maana nasema wanasuasua sana.
 
Daraja la waenda kwa miguu katika jiji la Mwanza na hususan katika Eneo la mabatini ni mpango ulio ibuliwa na watendaji wa serikali katika Vikao vya ushauri vya Mkoa (RCC), ilikukomesha adha ya Msongamano wa magari katika mji wa Mwanza.
 
Daraja hilo linajengwa na kampuni ya, NODIC Constraction, aidha kukamilika kwa daraja hilo itakuwa ni mwarobaini wa msongamano wa magari kwa magari yapitayo katika njia hiyo ya Nyerere na kuwezesha wananchi wa mji wa Mwanza kuwahi kazini Nyakati za asubuhi na Nyakati za jioni.
 
 
 
 
Mkoa wa Mwanza ambao hivi sasa Unajumla ya watu Mil. 2.7na zaidi kwa mujibu wa sense ya watu na Makaazi ya mwaka 2012, ni moja ya miji ambayo inanyemelewa na msongamano wa magari kutokana na kuwa na bara bara tatu tu zinazo ingia na kutoka jijini humo, ambazo ni Nyerere, itokayo Musoma na Nchi jirani ya Kenya, Kenyata yenye kutokea Shinyanga na Mikoa ya Geita na Simiyu ambayo ndio njia kuu yakupitisha magari yatokayo Dar- Es Salaam na ile ya Uwanja wa Ndege.
 
Mwanza ni mji unaokuwa kwa kasi kusini miongoni mwa miji iliyopo kusini mwa  Jangwa la Sahara na unatajwa nji wa pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ukitanguliwa na DSM.
Axact

Post A Comment: