Na Rajab Ramah, Nairobi.

Utengaji wa baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika utekelezaji wa mipango ya muungano kunaweza kusababisha kuvunjika kwa jitihada za muungano kamili wa kanda, wachambuzi wasema.

 

Kutoka kushoto kwenda kulia, Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete wakitembea pamoja wakati walipowasili kwenye mkutano wa kawaida wa 14 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Nairobi tarehe 30, 2012. [Tony Karumba/AFP]

Wakuu wa usalama kutoka Uganda, Kenya na Rwanda walikutana mjini Kigali, Rwanda mapema mwezi huu ambapo walitia saini mkataba wa usalama na ulinzi kurahisisha harakati za raia na watalii za kutoka sehemu moja kwenda nyingine katika kanda unaolenga kuongeza biashara kati ya mpaka wa nchi moja na nyingine.

Mkutano huo wa tarehe 9 Januari wa maofisa wa jeshi, polisi, upelelezi na uhamiaji umefuatia uanzishwaji wa visa ya pamoja ya utalii na nchi hizo tatu ambayo ilianza rasmi tarehe 1 Januari.

Hii ilikuwa ni mara ya nne viongozi hao wa Uganda, Kenya na Rwanda kufanya makubaliano kuhusu masuala ya muungano pasipo ushiriki wa Tanzania na Burundi, ambazo pia ni mwanachama wa muungano huo wa nchi tano.

Tanzania na Burundi hazikuhudhuria mkutano uliofanyika Uganda na Kenya mwezi Agosti mwaka uliopita, au mkutano uliofanyika huko Kigali mwezi Oktoba 2013.

Tanzania ililalamika kutengwa katika mazungumzo, na rais Jakaya Kikwete alisema, "Wameunda umoja wa hiari. Nani ambaye hana hiari?"

Kuvunjika Jumuiya ya Afrika Mashariki siku zijazo?

Katika Mkutano wake wa Kawaida wa 15 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Wakuu wa Nchi huko Kampala mwezi Novemba mwaka jana, viongozi walisema watajitolea kufanya kazi pamoja, lakini wachambuzi wa mambo wanasema kuwa hakuna uwezekano wa kutokea hilo.

"Nina wasiwasi kama wakuu wa nchi tatu -- Museveni, Kenyatta na Kagame -- walikuwa makini wakati wa mkutano kuhusu ahadi yao ya kusaidia wanachama wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika shughuli zao kwa sababu kinyume na azimio lao walikuwa Rwanda peke yao," alisema Rais wa Chama cha Sheria Afrika Mashariki (EALS) James Aggrey Mwamu. "Huo ni uthibitisho wa kutosha kwamba wanajitoa kufanya kazi bila ya Tanzania na Burundi."

Makubaliano ya pande tatu ni tishio kwa mtangamano wa kanda kwa kuwa yanazitenga kwa makusudi Tanzania na Burundi, alisema.

"Kile tunachokiona kinachoitwa hatua ya 'muungano wa hiari' ni ujengaji wa wingu la wasiwasi na jambo baya miongoni mwa nchi wanachama ambavyo vinaweza kuchochea mgawanyiko na kupanda mbegu ya kutoelewana ikisababisha kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kama ilivyofanya mwaka 1977," Mwamu aliiambia Sabahi. "Kwetu sisi, 'muungano huo wa hiari' haukubaliki kwa kuwa ni kinyume na mkataba ambao uliiunganisha Jumuiya ya Afrika Mashariki."

Kushindwa kwa nchi zote wanachama kuungana katika mipango ya pamoja kisiasa na kimaendeleo ni sawa na kuiacha kanda isambaratike, alisema.

"Kwa sasa kanda inakabiliwa na changamoto nyingi zikianzia katika kukosa utulivu wa kisiasa, uharamia na ugaidi, kwa hiyo, [hatutarajii] kuwatenga wengine na kuhisi kwamba tutafanikiwa," Mwamu alisema, akiwaomba viongozi wa kanda kushauriana mara kwa mara ili wasiendelee kufanya makosa.

Mgawanyiko wadhoofisha mshikamano wa kanda

Ingawa kujumuika pamoja kunachukuliwa kuwa bora na viongozi wa kanda walio wengi, Tanzania imepata sifa ya kutoharakisha masuala ya mtangamano na Burundi inachukuliwa kama nchi isiyo na chochote cha kutoa, alisema George Omondi, mwandishi wa habari wa gazeti la The East African anayeandika kuhusu masuala ya kanda.

"Tanzania imekuwa ikiibua masuala ya umiliki wa ardhi, shirikisho la kisiasa na uraia ambavyo inataka mwongozo ulio wazi, lakini washirika wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, badala ya kukaa chini kutatua hili, wanaliona kama dalili ya kuleta mvutano," Omondi aliiambia kuninews"Wamechagua njia iliyo rahisi zaidi, ambayo ni kujitenga, [na] ambayo sio sahihi."

"Burundi inaonekana kama mshirika masikini ambaye hana thamani katika mtangamano hivyo wanachagua kuipuuza wakisahau kwamba nchi ina watu zaidi ya milioni 9 ambayo inaweza kwa urahisi kuwa soko kwa bidhaa za Kenya, Uganda au hata Rwanda," alisema.

Manu Chandaria, mfanyabiashara wa Kenya na mwenyekiti wa Kundi la Comcraft ambalo linazalisha bidhaa za chuma, plastiki na aluminiamu katika Afrika Mashariki, alisema mgawanyiko wa hivi karibuni utadhoofisha ufanikishaji wa malengo ya mtangamano wa kanda yaliyowekwa.

"Sisi katika sekta ya biashara tunahisi kuwa kuvunjika tena au kujitenga kutaanzisha vikwazo vipya katika biashara," Chandaria aliiambia kuninews. "Kila nchi inaanzisha na kutumia mifumo yake tofauti ya biashara … itakuwa ni pigo kwa biashara huria ambazo tumekuwa tukikabiliana nazo muda wote huu."

Ili kufurahia kikamilifu faida inayotokana na umoja wa forodha na itifaki ya soko la pamoja, na kukamilisha uanzishaji wa fedha ya pamoja na shirikisho la kisiasa, alisema viongozi wa kanda hiyo wanapaswa kuvumiliana na kuwa tayari kushughulikia masuala ya msingi.

Kuiacha nchi moja nyuma kutazuia mchakato mzima, alisema.

"Tunachokiona ni kutokuwa na uvumilivu kwa baadhi ya viongozi. Hatuwezi kudhani kwamba tutaendelea kwa kuwaacha wale walioibua maswali kuhusu mchakato," alisema Chandaria. "Wangepaswa kukaa na kujaribu kutatua matatizo yaliyoibuliwa na Tanzania badala ya kuamua kuendelea."

EAC imeungana na ni yenye malengo, asema Kandie

Kwa upande wake, Katibu wa Wizara ya Masuala ya Afrika Mashariki Kenya Phyllis Kandie alipinga hisia za kujitenga, akisema muungani wa EAC utafanyika kama ilivyopangwa.

"Sitapenda kuingizwa katika mjadala huo 'muungano wa hiyari', lakini ninachoweza kukueleza ni kwamba sisi ni muungano kama tulivyokuwa awali na kwamba tuna malengo ya kufanikisha misingi ya EAC," Kandie aliiambia Sabahi.

Katika kujibu swali la iwapo mikutano ya nchi hizo tatu zinapingana na mkataba wa EAC, alisema, "Uganda, Kenya na Rwanda wanatumia utengano wa nchi kadhaa ambayo imeelezwa katika mkataba."

Utengano huo ni msingi katika Kifungu cha 7 cha Mkataba wa EAC, ambacho kinaruhusu maendeleo katika umoja miongoni mwa kundi dogo la wajumbe katika muungano mkubwa katika maeneo tofauti na katika kasi tofauti.

Hata hivyo, chini ya kifungu hicho, nchi wanachama ambazo zinataka kuendeleza kwa haraka bado zinatakiwa kuwafahamisha wajumbe wengine, ambalo halijafanyika katika suala hili, kwa mujibu wa Mwamu.

Jaribio la kumpata Katibu Mkuu wa EAC Richard Sezibera kwa ajili ya maoni halikufaulu

 
Axact

Post A Comment: