MWALIMU 
wa   kujitegemea   ambaye  pia  aliwahi 
  kuwa  Mchungaji  wa  Kanisa  la Kiinjili 
la Kilutheri  Tanzania(KKKT) mkaoni  hapa , Nicodemus  Mhana (
umri  wa zaidi  ya miaka 50) anakabiliwa na kashfa  ya
kubaka  mwanafunzi  wa  darasa  la 4(jina lake 
pamoja  na jina  la shule  anakosoma  vinahifadhiwa).
Habari  
zilizothibitishwa  Jeshi  la Polisi  pamoja  na
mwenyekiti  wa   Serikali  ya Mtaa  wa Msumbiji 
katika  Kata  ya Pasiansi  Wilayani  Ilemela, 
Fortunatus  Cheneko, zinasema Mhana  anadaiwa kutenda 
unyama  huo  Machi 4  mwaka huu.
Hata 
hivyo, inadaiwa kuwa  mtuhumiwa   huyo alikamatwa
  Machi 19 mwaka huu  na  Polisi   katika 
kituo kikuu cha  Wilaya  ya  Ilemela  (Kituo
 cha  Polisi  Kirumba), siku chache  baada  ya
baba  mzazi  wa mwanafunzi  huyo  kutoa  taarifa 
ingawa pia  alipewa  dhamana  siku  hiyo  hiyo 
kwa  madai  kuwa ana undugu   wa karibu  na
  maofisa  kadhaa  wa  Jeshi  la Polisi. 
Kwa  
mujibu  wa   habari, Mhana    alifanya 
ubakaji  huo  wakati   akiwa na mwanafunzi  huyo 
katika  kituo  chake  cha masomo  ya ziada 
kilichoko   katika  mtaa  wa Msumbiji.
Inadaiwa  
kwamba   Mhana  ambaye   mara  kadhaa 
amekuwa     akilalamikiwa  na baadhi  ya
wananchi   wa Mtaa  wa Msumbiji   kutokana  na
tabia  yake  ya  kupenda  kurubuni  watoto (wa
kike)  wadogo  kwa nia  ya kufanya nao mapenzi, alivuliwa 
Uchungaji  miaka  kadhaa  iliyopita  kutokana 
na  kukiuka  taratibu  pamoja  na maadali  ya kanisa .
 “ 
Cha   kushangaza  ni  kwamba  mtuhumiwa  alipewa
dhamana  siku  hiyo hiyo. Inagwa yeye(mtuhumiwa )  huku 
uraiani   anatamba  kuwa   hawezi  kufikishwa
mahakamani  kwa sababu  ana  ndugu  zake   wa
karibu  katika  jeshi  la Polisi  ambao  ni
wamezaliwa  katika  mkoa  wa  Singida” alidai baba 
mzazi  wa mtoto  huyo, Fredrick Mariba,  wakati  
alipoulizwa  na  JAMHURI , jana.
Anadai 
kuwa  alichelewa   kubaini  kuwa mwanaye  
huyo  mwenye umri  wa  miaka  11 amebakwa   kwa
sababu  baada  ya  kufanyiwa unyama  huyo  mtoto 
huyo  hakuweza   taarifa kwa  wazazi  labda  kwa
kuogopa  kuadhibiwa , hadi  alipohojiwa  na mama 
yake   wa kambo   pamoja  na bibi  yake kutokana 
na kulalamika maumivu  hasa anapokwenda  kujisaidia  chooni.
“
Ilibainika  siku moja   baada  yab kwenda 
kujisaidia  chooni   ambapo   alisikika  
akilia. Na  ndipo  bibi  yake  
alipomuuliza    na kisha   akamkagua   sehemu 
za  siri  na kubaini  kuwepo   kwa
michubuko”   alisema  na kuongeza  kuwa baada  ya
kuhojiwa kwa kina mtoto  huyo  alisema aliyekuwa  mwalimu 
wake kabla  ya kuanza darasa la kwanza, yaani  mwalimu 
Mhana  ndiyo  alimlazimisha  kufanya  mapenzi.
Huku  
akibubujikwa   na  machozi, Mariba  
alilalamika   kuwa   kitendo  cha askari Polisi 
kuruhusu  dhamana  kwa mtuhumiwa huyo  kabla  ya
kufikisha  suala  hilo mahakamani   kinaweza 
kuhatarisha  maisha  ya mtoto  wake.
“ 
Jambo  jingine  ni  kwamba hadi  sasa  Madaktari
  katika  Hospitali  ya Mkoa( Sekou-Toure) bado 
hawajathibitisha  chochote   kwa maandishi  iwapo 
mtoto  huyu  amebakwa  kweli  ama  la. Kila
nikienda  ninambiwa  mara  Daktari Mkuu  hayupo  
ama  yuko  bussy, kitendo  ambacho  kimesababisha 
mwanangu   ashindwe kwenda  shule  kwa  zaidi ya
majuma mawili sasa”  alisema.
Akizungumza  
na  gazeti   hili nyumbani  kwake  jana( Machi 
27), Mwenyekiti  wa  Serikali ya  Mtaa   wa Msumbiji,
Cheneko   alisema  kitendo  kinachodaiwa kutendwa na
mchungaji  huyo  kimezua  hofu  miongoni 
mwa   wakazi  wa mtaa  huo.
“ 
Kwa   ujumla  taarifa  hizi  zimeleta  hofu,
hasa   kwa wazazi  wa   wanafunzi 
wanaosoma  katika  shule  hii  kwa sababu  inawezekana
kabisa  kuwa wengi  wameshabakwa halafu  wakanyamaza.
Tunaomba    wahusika   wafanye  uchunguzi 
zaidi   dhidi  ya mwalimu  huyu  kwani  anaweza 
kusababisha  uvunjifu wa   amani  hapa mtaani 
kwetu  iwapo  mtuhumiwa  ataendelea  kutamba
  kwamba  yeye  hakamatiki  wala hawezi  
kufikishwa mahakamani“  alisema  Cheneko.
 Cheneko 
 aliendelea    kudai   kuwa baada  ya
kufuatilia  amebaini  kwamba  kituo  kinachomilikiwa na
mwalimu  huyo  hakina usajili  wowote.
Alisema 
ameshatoa  taarifa   hizo  katika  ofisi ya
 Mkaguzi  wa Elimu  wa  Manispaa   ya
Ilemela  ili kubaini  iwapo  kituo  hicho 
kimesajiliwa ama  la.
Hata 
hivyo,  jitihada  za JAMHURI    kumpata 
Mhana  ili  aweze   kuzungumzia   tuhuma 
zinazomkabili  bado    hazifanikiwa kwa sababu 
kituo  kimefungwa  tangu  juzi  na hata  
simu  yake  ya mkononi  ( 0756 018 147)inaonesha  kuwa
haipo  hewani.
“ 
Katika  kumbukumbu  zetu  hatuna  kituo   
kinachomilikiwa na mwenye jina  unalolitaja. Tumeshaambiwa   na
ndio  tunajiandaa  kwenda  huko  Msumbiji 
kufanya  ukaguzi  katika  kituo  hicho”  alisema
Mkaguzi Mkuu   wa Elimu   katika  Manispaa  ya
Ilemela, Leah Athanas, wakati   alipoulizwa  n JAMHURI .
Kamanda  
wa Polisi  mkoani  hapa, Valentino  Mlowola, alikiri  
kuwepo   kwa taarifa  hizo  na kwamba  ofisi 
yake  inaendelea  na uchunguzi.
Alisema  
ni  haki  ya mtuhumiwa kupata  dhamana  na
 atakamatwa  na kufikishwa  mahakamani  mara
 uchunguzi   utakapokamilika.
Kumbukumbu 
za Polisi(JAMHURI  limeziona)  zinaonesha  kuwa tukio 
hilo  liliripotiwa  katika  kituo  cha Polisi  Kirumba
siku  ya   Machi 19  mwaka huu  majira  ya saa 3:10
asubuhi( 09:10 hrs
 
 
Post A Comment: