Mamlaka ya usimamizi wa mifuko ya Hifadhi ya jamii ( Social Security Regulatory Authority) kwa kifupi (SSRA)  Wapo Jiji Mwanza kwa ajili yakutoa Elimu kwa umma juu ya Umuhimu kwa Watumishi na watu binafsi kujiunga na kujiwekea akiba katika Mifuko ya hifadhi ya Jamii.
 
Katika siku yao ya kwanza wametoa elimu kwa Wanafunzi wa chuo cha CUHAS- Bugando cha Jiji Mwanza na siku inayofuata wamepanga kutoa elimu kwa Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Jeshi la Polisi katika Mkoa huo pamoja TUCTA ambao ni Muunganiko wa vyama vya wafanyakazi
 
Kwa mujibu wa  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano SSRA Bibi Sarah Kibonde, amesema lengo la Semina hiyo kwa watumishi na wasio watumishi ni kuona  watu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla inaitambua mamlaka hiyo pamoja na shughuli zake ili wafanyakazi na wadau mbali mbali waweze kuitumia kama sehemu yakupeleka changamoto mbali mbali zilizomo kwenye mifuko tofauti tofauti ya hifadhi ya  jamii na kupatiwa majawabu.
 
Katika semina hiyo iliyo hudhuriwa na wanafunzi  zaidi ya 200 chuoni hapo,  baadhi ya changamoto zilizo ibuliwa  ni pamoja na baadhi ya mifuko ya hifadhi ya Jamii kutokuaminiwa na wanachama wake kwakutowasilisha michango kwenye mfuko wa mwanachama, jambo ambalo Bibi  Kibonde aliahidi kulichukua na kulipeleka kenye mamlaka husika kwa ajili yakutafutiwa ufumbuzi.
 
Habari na Picha  zote  na.  Atley Kuni-Afisa Habari Mwanza. 
 
TAZAMA PICHA ZAIDI HAPA...
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhamasihaji Bi.SARAH KIBONDE MSIKA akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha CUHAS -BUGANDO kuhusu umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii




UKUMBI UKIWA TULI KWA UMAKINI MKUBWA WAKIMSIKILIZA  BIBI SARAH KIBONDE, HAYUPO PICHANI WAKATI WA SEMINA HIYO.

SARAH KIBONDE MKUU WA MAWASILIANO WA SSRA, AKITOA SEMINA KWA WANAFUNZI WA CUHAS- BUGANDO JIJINI MWANZA.



MZEE RICHARD MASUNGA, AMBAYE NI MFANYAKAZI WA  BUGANDO AKITOA KILIO CHAKE MBELA YA  SSRA, HIVI KARIBUNI WALIPOFIKA KUTOA SEMINA KATIKA CHUO CHA CUHAS- BUGANDO.


MMOJA YA WANAFUNZI HUYU ALIPO SIMAMA KUTAKA KUJUA DHAMANA YA SSRA KATIKA KUDHIBITI MIFUKO HIYO.


MAKAMU WA RAIS CHUO CHA CUHAS- BUGANDO BW. ATUKUZWE GWIHANGWA, AKITOA UTANGULIZI WAKATI WA UGENI WA SSRA ULIPOZULU CHUONI HAPO HIVI LEO.


MAKAMU WA RAIS AKINUKUU JAMBO MUHIMU WAKATI WA SEMINA HIYO.

HAPA BW. LEBARATUS CHONYA  AKINUKUU BAADHI YA MASWALI KUTOKA KWA WANAFUNZI WALIO HUDHURIA SEMINA HIYO.


BWANA WILLFRED PASCHAL AKIULIZA SWALI KATIKA SEMINA HIYO, LAWAMA ZAKE AKIZIELEKEZA ZAIDI KWENYE MFUKO WA HIFADHI WA JAMII WA   NSSF.

BW. LIBERATUS CHONYA AMBAYE NI AFISA UHUSIANO MWANDAMIZI WA SSRA, AKITOA  MAELEZO YA AWALI KABLA YA SEMINA KUANZA.

BIBI SARAH KIBONDE AKIJIBU BAADHI YA MASWALI YA WADAU HAWAPO PICHANI KUSHOTO NI MAKAMU WA RAIS WA  CHUO NA KULIA NI BWANA CHONYA MMOJA YA MAAFISA WA SSRA, WALIPOFIKA KUTOA SEMINA KATIKA CHUO HICHO.
 
Axact

Post A Comment: