Bibi Sarah Kibonde akitoa mada katika chuo cha CUHAS- Bugando cha Mwanza hapo jana. |
Mamlaka ya Udhiti na usimamizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini (SSRA), hii leo itatoa Semina kwa atendaji wa Serikali juu ya umuhimu wa Mifuko hiyo kwa mfanyakazi pindi anapo fikia umri wa kustaafu.
Akizungumza na kuniblog hapo jana, Mkuu wa mawasiliano wa mamlaka hiyo Bibi Sarah Kibonde alisema kwa muda mrefu watumishi wamekuwa wakijiunga na mifuko ya hifadhi ya Jamii lakini hawajui haki zao za msingi hasa pale inapotokea mtumishi amepata tatizo kwenye mfuko anao changia.
WANAFUNZI WA CUHAS- BUGANDO WAKISIKILIZA BIBI KIBONDE |
Bibi Sarah, alisema tangu kuanza kwa mamlaka hiyo, watumishi wengi hawajapata fursa ya kuijua mamlaka na hivyo pamoja na mambo mengine watakayofanya kama mamla ni kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii ili waweze kuitambua mamlaka hiyo.
Mbali na Watumishi kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa watakao patiwa elimu hiyo hivi leo, watu wegine wanaotegemewa kupatiwa elimu hiyo ni pamoja na Askari wa Polisi, Muungano wa vyama vya wafanyakazi (TUCTA), vyuo vya Elimu ya juu pamoja na wajasiriamali.
Na: Atley Kuni- Afisa Habari RS Mwanza.
Post A Comment: