Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia Watanzania  wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,324 ambazo ni  kwa ajili ya waajiri mbalimbali Nchini.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi amesema kuwa nafasi 1,334 zimeainishwa bayana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz  ili kuwawezesha wahitimu wote wenye sifa na uwezo kutuma maombi kwa ajili ya kujaza nafasi hizo ajira Serikalini.
"Nadhani ni vizuri zaidi kwa kila muhitimu anayetafuta kazi serikalini kufungua tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kuangalia nafasi za kazi zilizotangazwa na pale anapoiona kazi inayoendana na sifa alizonazo kutuma maombi yake ili kuweza kushindanishwa na wengine....maana ajira za Serikali hivi sasa ni za ushindani hivyo inampasa kila anayetaka kupata kazi serikalini kujiandaa vyema ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kuajiriwa katika Utumishi wa Umma" alisema Daudi.
Alifafanua kuwa kwenye tovuti hiyo kuna matangazo mawili tofauti ya kazi ambapo moja liko katika lugha ya Kingereza likiwa na jumla ya nafasi za kazi 447 na tangazo lingine lipo kwa lugha ya Kiswahili ambalo lina jumla ya nafasi za kazi 877.
Aidha, alizitataja baadhi ya nafasi hizo za kazi zilizoko katika tangazo la kazi kwa lugha ya Kiswahili kuwa ni Mhandisi kilimo (agro–engineers), Afisa kilimo (agro–officers) Mkufunzi kilimo (aquaculture), Afisa kilimo msaidizi (agricultural field officers), Daktari wa mifugo (veterinary officers), Daktari utafiti mifugo (veterinary research officer), Daktari mifugo mkufunzi (veterinary tutor), Mkufunzi mifugo (animal science), Afisa mifugo (live stock officer), Afisa utafiti mifugo (livestock research officer), Afisa Utumishi (human resources officer), Afisa ardhi msaidizi, Dereva (driver).

Nafasi nyingine ni pamoja na Afisa utalii, Afisa ushirika (cooperative officer), Afisa Serikali za mitaa (local government officer) Mhandisi ufundi (mechanical engineer), Mhandisi haidrojiolojia (hydrogeologists), Mhandisi (maji) – water resource engineer, Mhandisi (maji) – water resource with gis engineer, Mhandisi (umeme) Mhandisi mazingira (environmental engineer), Mhandisi kilimo (agro – engineers), Afisa kilimo (agro – officers), Mkufunzi kilimo (aquaculture), Afisa kilimo msaidizi (agricultural field officers), Daktari wa mifugo (veterinary officers), Daktari utafiti mifugo (veterinary research officer).

Kada nyingine ni  Daktari mifugo mkufunzi (veterinary tutor), Mkufunzi mifugo (animal science), Afisa mifugo (live stock officer), Afisa utafiti mifugo (livestock research officer), Afisa ardhi msaidizi, Afisa utalii, Afisa ushirika (cooperative officer), Ufundi (technician mechanics), Fundi sanifu - ufundi (technician mechanics), Fundi sanifu - umeme (technician electrical), Fundi sanifu  – (water works technician), Fundi sanifu maabara– (water laboratory technician), Fundi sanifu - maji - (technician- water),Fundi sanifu msaidizi (ufundi bomba) - (assistant water works technician plumbing).

Wengine ni Fundi sanifu msaidizi (upimaji ardhi) - (assistant water works technician geometric), Fundi sanifu msaidizi mitambo ya maji (pampu),Fundi sanifu msaidizi mitambo ya maji (umeme), fundi sanifu msaidizi - (assistant technician welding), Mhandisi - ujenzi  (engineer– civil), Fundi sanifu – ramani (technician - (mapping) na Mpiga chapa msaidizi (assistant printer) .


Kwa upande wa Tangazo la Kingereza kazi zilizotangazwa ni pamoja na "Senior research engineer", "Research engineer assistant", "Principal engineer", "Engineer", "Artisan", "Chief accountant", "Human resource development and administrative manager", "Human resource development and administrative officer", "Welder", "Tutor", "Principal planning and promotion officer", "Director of planning, finance and administration", "Tutors (travel & tourism), "Supplies officer", "Mediator", "Arbitrator", "State attorney", "Personal secretary"," Office assistant", "Security guard", "Receptionist", "Transport officer", "Law secretary", "Computer system analyst", "Librarian assistants", "Procurement specialist", "Director of nutrition policy and planning", "Assistant medical officer", "Director of finance and administration", "Environmental management officer-science".

Daudi alifafanua kuwa nafasi hizo za kazi zilizo kwenye katika tangazo la lugha ya Kiswahili ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Shinyanga, Dodoma, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Rukwa, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Sikonge, Liwale, Handeni, Iramba, Sumbawanga,Iringa, Tanga, Ileje, Korogwe pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa.


Aliongeza kuwa kwa tangazo la kazi la lugha ya Kiingereza waajiri wake ni pamoja na Mamlaka na Bodi zifuatazo;- Tanzania Engineering and Manufacturing Design Organization (TEMDO), Tanzania Automotive Technology Centre (TATC), Ardhi Institute Morogoro, Tea Board of Tanzania (TBT), National College of Tourism (NCT), The Commission for Mediation and Arbitration (CMA), Attorney General’s Chambers, Tanzania Food and Nutrition Centre (TFNC), Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC), The National Environment Management council (NEMC) and The Cashewnut Board of Tanzania.

Katibu amesema Utumishi wa Umma unahitaji watu makini, wenye weledi katika taaluma zao na wenye maadili mema, kwa kuwa mtumishi wa umma ni kioo cha jamii anaetakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuiwezesha Serikali kutimiza malengo yake kwa ufanisi, ndio sababu ofisi yake inasisitiza waombaji wa kazi kujiandaa vizuri ili kuweza kushindana na wengine wenye uwezo kama wao. Hivyo, amewataka waombaji wa nafasi za kazi kutembelea wao wenyewe tovuti hiyo ya Sekretarieti ya Ajira ili kujua nafasi na daraja la kazi lililotangazwa ili kuepuka uwezekano wa kupewa taarifa za kupotoshwa na kuomba kazi ambayo haijatangazwa na kujikuta mwombaji akipoteza fursa ya ajira bila ya sababu za msingi.

Mwisho amebainisha kuwa mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi hizo zilizotangazwa ni tarehe 14 Julai, 2014 na kuwataka waombaji wote kuwasilisha maombi ya kazi kwa njia ya posta kwa kutumia anwani iliyowekwa katika matangazo ya kazi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 30 Julai, 2014.
Axact

Post A Comment: