PICHANI VIJANA HAWA WAENDESHA MKOKOTENI KAMA WALIVYO NASWA NA KAMERA YETU ENEO LA NYAKATO MECCO JIJINI MWANZA WAKISAFIRISHA MKAA, AMBAPO TAKWIMU ZINAONESHA ZAIDI YA ASILIMIA 64 WAISHIO MJINI WANATUMIA MKAA.

Takwimu zinaonesha zaidi ya 64% waishio mijini wanatumia mkaa utokanao na miti jambo ambali linatajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuharibu na kuchangia mabadiliko ya tabia ya nchi. Matumizi hayo sio kwamba yanachangia tu uharifu wa mazingira lakini pia suala la ukame nalo linazidi kuongezeka.
 
Akizungumza na mtandao huu, moja ya wafanyabiashara ya mkaa katika Jiji la Mwanza anasema takribani tani laki saba kila mwaka huvunwa na kuchomwa mkaa katika maeneo tofauti tofauti ya Mkoa huo wa Mwanza.
 
Hata hivyo wataalam wa Masuala ya mazingira kutoka mamlaka za serikali wanasema pamoja na jitihada zinazo chukuliwa na serikali bado kazi hiyo haiwezi kuwa na mafanikio endapo wananchi hawata badili tabia na kuanza kutumia nishati mbadala.
 
Kwa hali hiyo wanaiomba jamii kwa jumla kutambua umuhimu wa mazingiara na kuacha kukata miti hovyo ili jamii ya sasa na yabadae waweze kuishi katika Dunia yenye mazingira mazuri.

Axact

Post A Comment: