Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amekutana na viongozi wa dini pamoja watendaji wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kwa ajili yakuzungumzia suala la maendeleo ya Mkoa huo na wa kwanza kukutana nao walikuwa watendaji wa Sekretarieti Mkoa na badaye jioni viongozi wa dini.
· Awapa rungu watendaji, awaambia wasifanye kazi kwa mazoea.
· Viongozi wa Dini wakerwa na Uchawi, Ukame, na hali duni katika zao la Pamba.
· “Vijana wengi wana ndoto za kuhamia Mwanza kuwa Machinga”- Askofu AIC asema.
![]() |
SHEKHE HASSAN FEREJI WA MKOA WA MWANZA AKICHANGIA JAMBO KATIKA KIKAO KILICHO WAKUTANISHA VIONGOZI WA DINI NA MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO. |
![]() |
MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO AKIFUNGUA KIKAO NA VIONGOZI WA DINI MKOANI HAPA. |
![]() |
VIONGOZI WA DINI WAKIFURAHIA JAMBO, ANAYE PIGA MAKOFI NI KIONGOZI WA KANISA LA SDA, AITWAE BULENGELA. KUTOKA DAYOSISI YA NYANZA |
![]() |
ASKOFU ANDREW GULLE WA KKKT DAYOSISI YA MASHARIKI YA ZIWA VIKTORIA AKICHANGIA MADA KATIKA KIKAO HICHO. |
![]() |
KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA ALIYE SIMAMA FAISAL ISSA AKIWA ANATOA MUONGOZO JUU YAKUCHANGIA KATIKA KIKAO HICHO. |
KIKAO
NA WATENDAJI WA RS MWANZA.
Katika
kile kinachoonekana nikuendeleza
harakati za kuwakumbusha majukumu yao na kuwahimiza kuacha kufanya kazi
kwa mazoea, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo amekutana na watendaji wa
Menejimenti na kuwaagiza kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake
wabadilike na kutoa matokeo chanya kwa umma wa wana Mwanza.
Mulongo
alikuwa akizungumza katika kikao cha ndani kilicho wakutanisha wakuu wa
seksheni na vitengo wa sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kwa ajili yakuwaweka sawa
watendaji hao, amesema haipendezi Mwananchi asikie tu kwamba kuna suala la
Mkongo wa taifa lakini kiutendaji au kimatokeo Mwananchi huyo unakuta hajui
hata maana ya mkongo wa taifa “ Ndugu zangu tunafanya vitu vingi vizuri lakini
vitu hivyo hatuvitafsiri kwa Wananchi kwa maisha yao ya kila siku alisema
Mulongo na kuongeza kuwa “nilazima tuende kwa malengo ili kuweza kufikia
malengo tuliojiwekea”.
Mulongo
amesema kwa mfano, hata suala la score
card bado ni msamiati mgumu kwa mwananchi wa kawaida kwakuwa hajui ni kwa
namna gani unafanyakazi lakini pia namna unavyoweza kumsaidia.
Mulongo
amekwenda mbali zaidi na kusema kazi kubwa aliyo nayo Katibu Tawala wa Mkoa
pamoja na wataalam wa sekretarieti ni kuhakikisha yanapatikana maendeleo kwakusimamia
ipasavyo na kuelekeza Halmashauri za Wilaya nini wanapaswa kufanya katika kuwaletea
maendeleo Wananchi.
Huku
akisema kutokana na kutosimamiwa ipasavyo ndio maana Mkoa wa Mwanza na Halmashauri
zake katika kipindi cha 2010/2011 na kipindi/2012/2013 zilipata hati za mashaka
jambo ambalo linatia shaka juu ya usimamizi wa halmashauri hizo” Utaona katika
kipindi cha 2010/2011 sawa mlipata hati safi lakini katika kipindi cha
2011/2012 mkapata hati safi zenye msisitizo na 2012/2013 mkapata hati ya
mashaka ni dhahiri kwamba kuna mahali mlipo lega”.
Mbali
ya masuala ya hati chafu Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa Mkoa wa Mwanza vyanzo
vya mapato vipo vingi lakini havijaunganishwa vizuri huku akitolea mfano
waendesha Boda boda ambao amesema robo tatu ya waendesha boda boda hawalipi
kodi kwasababu yakutokuwepo kwa mfumo rasmi wakuwatoza “Our source collection
they are not formalize hence ¾ of revenue collection lost, eg. Machinga and
Boda boda” alisema Mulongo.
Sekta
nyingine alizo zigusia Mkuu huyo wa Mkoa ni pamoja na uwekezaji hasa kwenye
maeneo ya ardhi ambayo haijatendewa haki ipasavyo ambapo amesema hata kama
ardhi ya Mwanza ni ndogo lakini kama itawekezwa ipasavyo itasaidia Wananchi
kuondokana na umaskini “ kila mtu afanye kazi yake kiufasaha ili kuweza
kumuokoa Mwananchi wa Mkoa huu” alisema Mulongo. “ Mimi kama RC jeuri yangu ipo
kwenu ninyi hivyo mfanye mfanyavyo ninyi pamoja na RAS kuhakikisha tunasonga
mbele.
MKUTANO
NA VIONGOZI WA DINI
Mkoa,
mbali yakukutana na Wakuu hao wa seksheni vile vile jioni hii amekutana na
Viongozi wa Madhehebu ya dini Mkoani hapa kwa ajili yakufahamiana lakini pia
kujua ni kwa namna gani wote kwa pamoja watasaidia katika kusukuma gurudumu la
mandeleo. “ Jamani mimi leo nimewaiteni lakini sina ajenda kubwa ambayo ninyi
hamuijui, suala hapa ni maendeleo ninyi kama viongozi wa kiroho ndio wenye
watu, sasa tufanyeje ili tuweze kwenda mbele na kuinua Mkoa wetu? Naomba kila
mmoja wetu atapata nafasi yakuchangia”.
Wakitoa
mawazo yao, viongozi dini walisema
pamoja na ushirikiano, yapo mengi yakufanya lakini kwakuwa haiwezekani yote
yakafanyika kwa siku moja ni vema kuanza na machache na kadri muda utakavyokuwa
unasogea ndivyo watakuwa wanashauriana, ambapo Askofu Andrew Gulle wa KKKT
Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria, alikuwa wa kwanza kusema na kumshauri
Mkuu huyo wa Mkoa kudumisha umoja uliokuwepo wakati wa uongozi wa aliyekuwa Mkuu
wa Mkoa aliyepita Mhandisi Evarist Ndikilo.” Mhe. Mkuu wa Mkoa mimi ninalo moja
nalo ni kuwa kupitia ule umoja wetu ambao tuna viongozi 20 kutoka pande zote
mbili za dini zetu hizi sisi tutakupa ushirikiano wakutosha”.
Katika
kikao hicho, viongozi hao wa dini wamemshauri Mkuu wa Mkoa kurudisha heshma ya
zao la pamba katika Mkoa huo kwakuwa, zao hilo ndilo lilikuwa mkombozi wa watu
wa kanda ya Ziwa ukiwapo Mkoa wa Mwanza “Mkuu wa mkoa hivi sasa kuna shida
kubwa sana ya ajira na vijana wote wanawaza kukimbilia Mwanza au Dar es salaam,
huku wakiwaza kuwa ndio kuna maisha bora kwakuwa huko vijijini hakuna kazi” alisema
mmoja ya maaskofu wa AICT.
Kwa
upande mwingine viongozi hao wamemuasa Mkuu wa Mkoa kukomesha suala la milio ya
mabomu, kushirikina, ulevi, uharibifu wa mazingira wa kupindukia ambavyo
imekuwa kero kubwa kwa Mkoa huo “Mkuu wa mkoa sula la mazingira bado nalo ni
shida, hivi sasa chakula kwa Mkoa huu tunategemea Wilaya ya Sengerema pekee,
tofauti na miaka ya nyuma” walisema viongozi hao wa dini
Naye
Askofu Sekelwa, akichangia katika kikao hicho aliamua kutoa kilio kwa watendaji wa Halmashauri ya Jiji na kusema “
Suala la Bilioni 40 katika Jiji la Mwanza ambazo zinatajwa zimefisadiwa, limefanya hata watu washindwe kuelewa endapo
kuna viongozi waliopewa dhamana yakuwasimamia watu, alisema Sekelwa na kuongeza
tunakuomba mkuu wa mkoa suala hilo ulichukue na ulifanyie kazi, haingii akilini
mamlaka zipo halafu fedha kiasi kiukubwa kiasi hicho zinapotea kienyeji, kweli
ni suala lisilo leta afya mbele ya jamii” alisisitiza askofu huyo
Mkoa
wa mwanza ambao unatajwa kuwa moja ya mikoa inayo changia kwa kiasi kikubwa
katika pato la Taifa, bado umekumbwa na changamoto kubwa ya ukusanyaji mapato
na hivyo kumfanya mkuu wa mkoa kuwa na mikutano na makundi mbali mbali katika
mkoa huo, aidha hivi karibuni anakusudia kukutana na wakuu wa Taasisi zilizopo
mkoani hapa kwa ajili yakuzungumza nao kuona ni kwa jinsi gani wanaweza kukuza
uchumi wa mkoa huu.
Post A Comment: