. Yazipiku Nyamagana, Ilemela.
. Yafaulisha kwa asilimia 78.9
. Magu yaing'ang'ania nafasi ya tatu.![]() |
KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA, DK. FAISAL ISSA ALIPOKUWA AKIFUNGUA KIKAO HICHO CHA KUTANGAZA MATOKEO. |
Wilaya ya Ukerewe imeibuka kidedea katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2014 na kuzipiku wilaya za Nyamagana na Ilemela ambazo mwaka 2013 zilishika namba moja na mbili ambazo zilifikia ufaulu wa asilimia 74.6 kwa Nyamagana na Ilemela iliyo faulisha kwa asilimia 71.3, hali imekuwa tofauti kwa mwaka huu wa 2014 ambapo wilaya ya Ukerewe iliyongoza, imefikia asilimia 78.9 na kuzidi ufaulu wa mwaka 2013 wa Nyamagana iliyopata asilimia 77.2 na Ilemela asilimia 72.2 na kufanikiwa kuwa namba moja.
Wakati huo huo Ilemela imezidiwa na Wilaya ya Magu iliyoshika nafasi ya tatu kwa mwaka huu na kuisukuma Ilemela hadi nafasi ya nne na kuizidi kwa kupata asilimia 75.5 hali inayo chagiza kuwa huenda kama kasi hiyo itaendelea basi zipo dalili za wazi kuwa Wilaya za pembezoni mwa mji kuongoza katika miaka ijayo na Wilaya za mjini kushushwa katika suala la ufaulu.
Akitangaza matokeo hayo ya darasa la saba kwenye sekondari ya Mwanza hivi karibuni, Afisa Elimu wa Mkoa wa Mwanza, Mwalimu Hamis Maulid, alisema "Tarehe 10/9/2014 na 11/9/2014 mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi
ulifanyika hapa nchini. Mkoa wa Mwanza
ulishiriki katika zoezi hilo, na jumla ya
wanafunzi 54384 walitarajiwa kufanya
mtihani huo, kati yao wavulana walikuwa 25889
na wasichana ni 28495 anasema Wanafunzi wote
hawa ni kutoka katika jumla ya shule za msingi 891 zilizoshiriki mtihani huo" anasema Maulid na kuongeza kuwa, mbali ya Wilaya ya Ukerewe kuwa na ufaulu mzuri lakini pia imesaidia kuinua ufaulu wa mkoa mzima wa Mwanza ambao uko chini ya mpango wa Tekeleza sasa kwa matokeo makubwa (BRN) na kuifikia wastan wa asilimia 69.07 kutoka asilimia 57.9 za mwaka 2013 ongezeko la zaidi ya asilimia 10 ambalo sasa linakaribia tarajio la BRN la mwaka 2014 la ufaulu wa asilimia 72. hata hivyo mkoa unabakia katika kibarua kigumu cha kufikisha ufaulu wa asilimia 82 kwa mwaka ujao wa 2015
Mbali ya ufaulu huo mkoa pia umeweza kushika nafasi ya 3 kitaifa katika mikoa 25 na umefanikiwa kuingiza shule 19 bora kati ya shule bora 100, huku shule ya Mugini iliyopo Wilayani magu ya ikishika nafasi ya pili kitaifa na ya kwanza kimkoa.
![]() |
AFISA ELIMU MKOA AKIJADILIANA JAMBO NA KATIBU TAWALA MKOA WAKATI WAKUTANGAZA MATOKEO HAYO. |
Maulid pia anasema "Waliofanya mtihani huo kwa mwaka 2014 ni wanafunzi 53597 wakiwemo wavulana 25484 na wasichana 28113 sawa na asilimia 98.5 ya Wanafunzi
waliofanya mtihani huo amabao walianza
darasa la kwanza mwaka 2008 wakiwa jumla ya wanafunzi 72054 kati yao wavulana 35262 na wasichana 36792 Kwa hiyo waliofanya mtihani huu ni sawa na
asilimia 74.4 ya wanafunzi wote
walioandikishwa darasa la kwanza mwaka 2008". anasema Maulid.
Aidha Maulid, alibainisha kwamba ,wanafunzi ambao hawakuweza kufanya mtihani kwa mwaka huo wa 2014 ni kama ifuatanvyo, alisema "Kati ya
wanafunzi 54384 waliotarajiwa kufanya mtihani huo,
wanafunzi 787 hawakufanya mtihani huo kwa sababu
mbalimbali zikiwemo za utoro, kifo, ugonjwa, kuhama, na mimba kwa wasichana.
Idadi hiyo ni sawa na asilimia 1.46".
![]() |
BAADHI YA WATENDAJI KUTOKA WILAYA ZOTE ZA MKOA WA MWANZA WAKIFATILIA UTANGAZAJI MATOKEO KATIKA SHULE YA SEKONDARI MWANZA. |
![]() |
AFISA ELIMU MSINGI WILAYA YA UKERWE FIDES MUNYOGWA AKIELEZA SIRI YAKUFANIKIWA HADI KUSHIKA NAFASI YA KWANZA KIMKOA. |
Aidha mazoezi ya mara kwa mara pia yamechagiza katika kupata ufaulu huo " Mwenyekiti sisi Wilaya ya Ukerewe tumefanikiwa kulipa madeni ya walimu kwa kutumia fedha za ndani na kuawafanya walimu waliokuwa wanadai waweze kuifanya kazi yao kwa moyo" anabainisha bibi Munyogwa.
Imeandaliwa na Afisa Habari. Mwanza RS.
Post A Comment: