JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

OFISI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA

 

 
TAARIFA KWA UMMA.


YAH: MLIPUKO WA UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE

 

Kumetokea mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya Nguruwe (African Swine Fever) Wilaya ya Nyamagana, Kata za Mabatini, Mirongo kishiri na Buhongwa na Igoma. Mlipuko huu umedhibitishwa kwa uchunguzi uliofanyawa na Maabara ya Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)

 

Ugonjwa wa Homa ya Nguruwe unasababishwa na Virusi (African Swine fever virus). Madhara yake ni makubwa kwa wafugaji na kiuchumi kwani husababisha vifo asilimia 100 (100%) kwa Nguruwe wote walioambukizwa.

Ugonjwa wa Homa ya Nguruwe hauna chanjo wala tiba na hauambukizi Binadamu. Njia pekee ya kudhibiti ugonjwa huu ni kuzuia kueneoa kwa maambuzi toka eneo lenye maambukizi kwenda eneo lisiloambukizwa.

HATUA  ZA TAHADHARI KUZUIA KUENEA KWA UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE

 

·         Wafugaji waepuke kununua Nguruwe kutoka kwenye Maeneo/Mashamba yenye ugonjwa

·         Nguruwe wafugwe kwenye Mabanda imara na waepuke kutembea ovyo

·         Nguruwe wasilishwe mizoga au masalio ya chakula kutoka vyanzo visivyojulikana

·         Teketeza Mizoga iliyokufa kwa ugonjwa na ufanye usafi kwa kuzingatia maelekezo ya watalaam na kwa kutumia dawa za kuua vimelea vya magonjwa (disinfectants)

·         Wakulima watoe taarifa ya uwepo wa ugojwa haraka kwa mtalaa wa Mifugo aliye karibu

·         Wananchi wazingatie maelekzo yote yanaotolewa pindi watalaam wa Mifugo wanapoweka Tangazo la Karantini (QUARANTINE) la kuzuka kwa   ugonjwa wa Homa ya Nguruwe

·          

IMETOLEWA LEO 11. DESEMBA, 2015.


Dkt Yohana D. Sagenge

Kny: KATIBU TAWALA (M)

MWANZA
Axact

Post A Comment: