Articles by "Vituko"
Showing posts with label Vituko. Show all posts
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba wakishangilia wakati mjumbe mwenzao, Joshua Nassari alipounga mkono kimakosa hoja ya kura ya wazi wakati anatoka upande unaoipinga. Picha na Salhim Shao
HAWA NDIO WABUNGE VITUKO.
Hali ya hewa jana ilichafuka kwenye Bunge la Katiba baada ya mjumbe Ezekiel Wenje kuwatuhumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda na baadhi ya mawaziri kuwa waliwahonga baadhi ya wajumbe wa kundi la 201.
Katika tuhuma hizo, Wenje alimtaja Waziri Profesa Jumanne Maghembe, Dk. Shukuru Kawambwa na Gaudensia Kabaka akisema kuwa walitoa rushwa ya vyakula, maji na vinywaji kwa wajumbe hao ili waunge mkono msimamo wa serikali mbili.
Kauli hiyo, iliyotolewa katika mjadala wa mabadiliko ya kanuni, ilisababisha mawaziri hao kunyanyuka kujibu tuhuma hizo, huku Wenje akisisitiza kuwa aliyoyasema ni kweli tupu.
Vilevile baadhi ya wajumbe wanaotoka katika kundi hilo walicharuka na kujaribu kujitetea huku mmojawapo akitishia kuwa iwapo Wenje asingeomba radhi, asingetoka ndani ya Bunge hilo.
Hoja ilipoanzia
Wenje, ambaye pia ni mbunge wa Nyamagana (Chadema), alianza kwa kueleza kwamba wapinzani "walilia" sana kuwa Bunge la Katiba lisingekuwa na usawa kutokana na Chama cha Mapinduzi kuwa na wajumbe wengi, ndipo ikaonekana wapatikane wajumbe wengine 201, lakini jambo la ajabu ni kwamba walioteuliwa katika kundi hilo asilimia 80 ni makada wa CCM akiwamo mzee maarufu ambaye ameingizwa kama mganga wa jadi.
Ingawa hakumtaja jina, Wenje alikuwa anamaanisha kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru aliyeteuliwa kupitia kundi la waganga wa jadi.
Kuhusu rushwa, Wenje alisema:"...Sasa kuna wajumbe wa kundi la 201 walipelekwa kwa Profesa Maghembe na Dk. Kawambwa wamepeana rushwa, vikao vingi vilifanyika usiku. Hii haikubaliki."
Baada ya kauli hiyo ya Wenje, Profesa Maghembe alisimama ghafla huku akionekana kutaharuki, ambapo Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan alimpa nafasi ya kujieleza.
Profesa Maghembe alikiri kuwakaribisha baadhi ya wajumbe wa kundi hilo, akieleza kwamba ilikuwa ni katika hali ya ukarimu uliozoeleka miongoni mwa jamii ya Kitanzania.
"Kuna kundi lipo hapa ambalo linafanya kazi ya kudhalilisha wenzao. Ni kweli niliwaalika kwa chakula wajumbe hao kwa taratibu za kawaida, lakini hakuna mbunge hapa anayeshindwa kujinunulia chakula, hakuna anayeweza kupewa rushwa.
"Kwa sababu hiyo ninaomba kiti chako kimtake mjumbe aliyewasilisha hoja hiyo aniombe radhi. Wenje aniombe radhi," alisema Profesa Maghembe akiwa katika hali ya hasira, huku kukiwa na sauti za kuzomea na kushangilia kutoka kwa wajumbe.
Makamu mwenyekiti pia alifanya jitihada za kuwataka wajumbe kuwa wavumilivu, huku akitoa nafasi kwa Dk. Kawambwa kujieleza akisisitiza kwamba ni tuhuma nzito.
Kawambwa alisema: "Ni kweli nilikutana nao; ni wajumbe ambao wanatoka kwenye taasisi zinazojihusisha na masuala ya elimu, lakini mbona wameshafanya mikutano yao mingine mingi ambayo mimi hawakuniita. Kama mtu akiwa hana hoja bora akae chini."
Makamu Mwenyekiti alimtaka Wenje aombe radhi kutokana na kauli yake, lakini katika hali ya kushangaza mjumbe huyo alisisitiza kwamba Profesa Maghembe na Dk. Kawambwa wamekiri.
"Maghembe amekiri aliwaita wafugaji na wavuvi ndiyo waliokula chakula cha rushwa, pia wapo wengine walienda kwa Waziri Gaudensia Kabaka, kuna ushahidi mama mmoja siwezi kumtaja jina hapa alikwenda huko akafukuzwa, nitakupa jina lake mwenyekiti baadaye. Aliambiwa kwamba anatoa siri... hoja iliyojadiliwa huko ilikuwa ni kwamba msimamo ni wa serikali mbili... rushwa ya chakula, maji na bahasha walipewa," alisema Wenje na kusababisha kulipuka kwa kelele zaidi.
Wenje aliongeza kuwa kuna wajumbe wengine walikwenda hadi kwa waziri mkuu ambako walikula, walikunywa hadi saa 7:00 usiku.
Alisema wengine walikwenda kwa Gaudensia Kabaka (Waziri wa Kazi na Ajira) na walikula na kunywa na kupewa bahasha.
Baada ya Wenje kukaa, baadhi ya wajumbe wa kundi la 201 walichachamaa wakitaka kutetea hadhi yao, akiwamo mjumbe kutoka kundi la wafugaji, Esther Juma aliyesema hawatendewi haki kama kundi kusema kwamba walihongwa.
Alisema yeye ana ng'ombe 3,000 na asingeweza kwenda kupokea rushwa ya chakula na kumtaka mbunge huyo kuwaomba radhi la sivyo asingetoka mlangoni.
Wakati mjadala huo ukiendelea, mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta aliyekuwa ametoka kwa udhuru, alirejea kimya kimya, na kumtaka Wenje kueleza iwapo anadhani kauli yake haikuwaudhi baadhi ya wajumbe.
Wenje alikiri kuwa ni kweli baadhi ya wajumbe wameudhika kutokana na ukweli aliosema dhidi yao na kuwaomba radhi kwa ukweli huo.
Kauli hiyo ilimfanya Sitta kutangaza kuwa anapeleka suala hilo kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge na uamuzi utakaotolewa atautangaza bungeni.
CHANZO MWANANCHI
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kati ya mambo ambayo yamewahi kuwashangaza watu katika ulimwengu wa jumuiya ya Kikristo, ni hatua ya mchungaji Jamie Coots wa kanisa la Full Gospel Tabernacle in Jesus Name, ambaye alikuwa akihubiri kwa kutumia nyoka, na kusema kuwa kuna ukombozi kupitia nyoka huyo.


Siku zimeenda naye akaendeleza injili hiyo ya nyoka, ambapo mwisho wa siku ameripotiwa kufariki baada ya kung'atwa na nyoka akiwa madhabahuni kanisani kwake.

Siku zimeenda naye akaendeleza injili hiyo ya nyoka, ambapo mwisho wa siku ameripotiwa kufariki baada ya kung'atwa na nyoka akiwa madhabahuni kanisani kwake.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea siku ya Jumamosi, ambapo alikuwa akihubniri madhabahuni, kabla ya nyoka kumng'ata, jambo ambalo alilichukulia kawaida na kukataa kwenda hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Mkuu wa polisi wa Middlesboro, eneo ambalo mchungaji huyo alikuwa akiishi, Jeff Sharpe, amesema kuwa mchungaji Coots alifariki kwenye majira ya saa nne usiku baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani kwake, ambapo aliondoka kanisani punde tu kabla ya watu wa huduma ya kwanza kufika kwa ajili ya kumhudumia na kumkosa mida ya saa mbili na nusu usiku - kisha wakanyookea nyumbani kwake ili kumpatia huduma, ambapo aliwakataliwa - nao wakaondoka maeneo hayo majira ya saa tatu na dakika kumi usiku.



video inayoonesha namna alivyokua akifanya ibada zake ni hii hapa chini.

Mara baada ya kuondoka, baadae walipokea siku kuwa mchungaji Coots amefariki dunia nyumbani kwake kutokana na sumu ya nyoka ambaye alimng'ata kwenye mkono wake wa kulia.

Mchungaji Coots ambaye amezaliwa mwaka 1971, amewahi kunusurika kufariki mara mbili, ambapo mwaka 1990 na 1998 aliwahi kuumwa na nyoka kwa nyakati tofauti, kwenye mkono wa kushoto na pia kwenye kidole cha kati cha mkono wa kulia, ambapo mara zote hizo alikataa msaada wa kitabibu.

Mwaka 1995, Bi Melinda Brown wa Parrotsville alifariki dunia baada ya kuumwa na nyoka kwenye kanisa la mchungaji Coots, ambapo polisi waliamua kumfungulia mashtaka Coots, hadi pale jaji alipotoa hukumu kumuachia huru, akitaka asisumbuliwe kutokana na imani yake.

Swali hapa mtaani ni kwamba, baada ya kufariki huyu mchungaji sijui ndo ameenda kwa nyoka ama wapi, anasikika akisema kijana mmoja mtaani.

Mchungaji Coots amekuwa akiendesha vipindi kupitia kituo cha runinga cha National Geographic, kiitwacho Snake Salvation, ambao wametoa tamko siku ya Jumapili la kusikitishwa na kifo cha mchungaji huyo, huku

 ukiwa umeshapata wadau (likes) zaidi ya 1,600 ambapo michango imekuwa ikiombwa kwa maelezo kuwa mchungaji huyo hakuwa na bima katika huduma yake hiyo.

Credits:gospel kitaa blog
   
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Mike "Iron" Tyson-Bingwa wa zamani wa uzito wa juu katika masumbwi

Bingwa wa zamani wa ngumi asiyepigika wa uzito wa juu Mike Tyson amesema anajisikia furaha baada ya kufanya upasuaji uliofanikiwa wa kubadilisha jinsia.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

WATU HAWATAKI KUFANYA KAZI WAMEBAKIA KUPIGA SOGA ASUBUHI YA SAA 2,00 HADI JUA LINWAKA UTWAKUTA TU . HAPO KEMONDO, STORI ZAO ZOTE NIKUISEMA SERIKALI KWA NAMNA HII KWELI TUTAFIKA?
no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Watangazi wawili wa Australia waliopiga simu ghushi hospitalini alipokuwa amelazwa mkewe Prince William, ambaye ni mjamzito wamesema wamehuzunishwa sana na kifo cha muuguzi aliyepokea simu hiyo.
Jacintha Saldanha alikutwa kafariki siku tatu baada ya kupokea simu iliyokuwa inaulizia kuhusu hali ya Duchess wa Cambridge, aliyekuwa hospitalini akiuguzwa ugonjwa unaohusika na mimba yake.
no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Wanuswa kwapa kama mahojiano
Hata ujuzi pia hauna maana.
Huko ni China.
Shirika maarufu la Uchina, HAINAN AIRLINE limeweka masharti kwamba mbali na elimu na uzoefu
lazima usinuke. Ukiwa mwili wako una harufu mbaya basi kazi huna. Ni China huko.
Kwa mujibu wa gazeti la SZ News shirika hilo katika kuajiri marubaNi wapya lazima mtu ananuswa
makwapa.