HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. FENELA MKANGALA
(MB), WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA
MICHEZO SIKU YA UZINDUZI WA BODI YA USHAURI YA
CHUO CHA MAENDELEO YA MICHEZO MALYA TAREHE 11/
12/2012.

Ndugu amawenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo;
Ndugu Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Chuo;

Ndugu Mkuu wa Chuo;

Ndugu Wana Jumuia ya Chuo;

Wageni waalikwa,

Mabibi na Mabwana.

Awali ya yote, naomba nimshukuru mwenyezi Mungu kwa
kutuwezesha sisi wote kufika hapa Chuo cha Maendeleo ya
Michezo Malya tukiwa salama salimini. Pili, nichukue nafasi hii
kuwapongeza ninyi nyote kwa kuteuliwa kwenu kuunda Bodi ya
Ushauri ya Chuo hiki, na zaidi kukubali uteuzi, hali inayoonyesha
jinsi mlivyo na mapenzi mema kwa Wizara yangu na ari ya
kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya michezo nchini.
Tatu, niwashukuruni nyote kwa kukubali mwaliko wetu, pamoja
na shughuli nyingi mlizonazo na kwa taarifa ya muda mfupi
mmeweza kujihimu na kufika hapa leo. Kusema kweli imenipa
faraja kubwa na hii inaonyesha jinsi ambavyo mnathamini
shughuli za Wzara yangu na hususani Sekta ya Michezo na zaidi

1

chombo hiki ambacho ni muhimu sana katika maendeleo ya Chuo
na maendeleo ya michezo hapa nchini kwa ujumla wake. Asanteni
na nawashukuru sana.

Ndugu Mwenyekiti,

Nisingependa niirudie historia ya Chuo kwa kuwa Mkuu wa Chuo
ameshaizungumzia katika taarifa yake. Ninachoweza kusema
katika hili ni kusisitizia tu kuwa Serikali imefanya juhudi kubwa
ya kukiendeleza Chuo hiki tangu ilipokabidhiwa na uongozi wa
Serikali ya Mkoa.

Hata hivyo, pamoja na jitihada za kukiboresha, tumeendelea
kukabiliwa na changamoto kadhaa na hasa zinazotokana
mabadiliko makubwa ya uchumi wa taifa na dunia kwa ujumla.
Baadhi ya changamoto zimeelezwa katika taarifa ya Mkuu wa
Chuo. Kwa jumla, mabadiliko hayo ya kiuchumi yamezidi kuifanya
sekta ya michezo kuendelea kuwa tegemezi zaidi kwa Serikali
hasa katika upande wa maendeleo ya taaluma ya michezo na
maendeleo ya miundombinu. Wakati mabadiliko hayo ya kiuchumi
yametia msukumo Sekta binafsi na sekta nyingine za umma kutoa
mchango kwa ukamilifu katika sekta nyingine kama vile Elimu,
Afya, Kilimo, Barabara na nyinginezo nyingi bado mchango wa
sekta hizo haujazama katika maendeleo ya taaluma ya michezo
pengine kwa kutofahamu nafasi ya michezo katika uchumi wa
taifa au umuhimu wa michezo kwa ujumla wake.

Ndugu Mwenyekiti,

2

Naomba niwakumbushe maneno ya Baba wa Taifa Hayati
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyowahi kusema alipokuwa
akifunga michezo ya majeshi mwaka 1978, nanukuu;

“Mazoezi ya mwili ni jambo la lazima kama kupumua.
Watoto, Vijana wetu na watu wazima lazima wajenge
tabia ya kufanya mazoezi ya mwili. Mazoezi ya mwili
humwezesha mtu viungo vyake kufanya kazi vizuri.
Michezo itumike kujenga miili imara na akili safi.” Mwisho
wa kunukuu.

Ndugu Mwenyekiti,

Wosia huo wa Baba wa taifa unanisukuma kuwahakikishia Ndugu
Wajumbe kuwa Serikali inayo nia ya dhati ya kuimarisha sekta
ya michezo kwa ujumla wake. Tunafanya hivyo kwa kutambua
umuhimu wa michezo kwa mtu mmoja mmoja, jamii na taifa kwa
jumla.

Sambamba na maneno haya ya Mwalimu, mtambue kuwa mnao
wajibu si tu kwa Chuo bali pia kwa jamii nzima kwa kuhakikisha
kuwa Chuo kinakua na kustawi ikiwa ni pamoja na kukitumia
na kukikuza kwa lengo la kuendeleza michezo ili kujenga taifa
lenye afya njema kupitia michezo. Vilevile, kwa kuwa michezo
ni biashara na ajira, siyo tu kwamba tutajenga Taifa lenye
afya njema, bali pia vijana wetu wanaweza kujipatia ajira na
kujiongezea kipato kupitia fani ya michezo.

Lengo la Serikali ni kupanua wigo wa ushiriki wa wananchi katika
michezo kama haki yao ya msingi, lakini kushiriki katika michezo
ilIyo bora ili hatimaye kadri ushiriki unavyoboreshwa tupate

3

wanamichezo wengi bora katika ngazi mbalimbali. Hata hivyo,
hatuwezi kufikia hatua hiyo kama hatutakuwa na wataalam bora
na wakutosha. Ili tuweze kutekeleza kwa ukamilifu maneno ya
Baba wa Taifa, tunahitaji kutoa taaluma ya michezo iliyo bora na
katika mazingira yaliyo bora.

Ndugu Mwenyekiti, uteuzi wenu umefanyika kwa kuzingatia
uwezo na uzoefu wenu katika kuendesha na kusimamia shughuli
mbalimbali za kitaifa. Mnakabidhiwa jukumu tukiamini kuwa
uzoefu wenu utaisaidia Serikali katika kuleta Maendeleo ya kweli
ya Chuo hiki. Uzoefu wenu utasaidia kwa pamoja kuunganisha
nguvu ya Serikali na Sekta binafsi katika kuboresha taaluma
na miundombinu ya Chuo. Weledi wenu utasaidia kuishauri
serikali namna bora ya kukiendeleza Chuo kupitia mpango
Kamambe[MASTER PLAN] ambayo tayari imeandaliwa.

Pamoja na matarajio hayo tuliyo nayo kutoka kwenu, mkiwa
Wajumbe wa chombo hiki muhimu katika maendeleo ya Chuo ,
mtakuwa na wajibu wa kutekeleza majukumu mbalimbali kama
ifuatavyo:-

I. Kusimamia ubora na uadilifu wa Chuo;
II.Kusimamia uendeshaji wa Chuo na kuwa kiungo muhimu
kati ya menejimenti ya Chuo na Wizara katika masuala
yanayohusu Sera;
III. Kushirikiana na Wizara kutafuta wabia wanaoweza
kuzaidia uboreshaji wa miundombinu ya Chuo ikiwa na
pamoja na viwanja vya michezo mbali mbali, nyumba za
watumishi, madarasa, mabweni, huduma ya maji safi na
vifaa vya kufundishia na kujifunzia;

4

IV.
Kusaidia katika kubuni na kutafuta vyanzo vya mapato
kwa ajili ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Chuo
kwa kushauriana na Wizara;
V. Kubuni mbinu za kuihusisha sekta binafsi na sekta ya umma
katika kuendeleza Chuo na utoaji huduma mbali mbali na
kuishauri Wizara kuhusu utekelezaji wake;
VI. Kuhakikisha kuwa Chuo kinakuwa na mazingira
yanayoruhusu uhuru na kujiamini katika kuhoji, kufikiri na
kuelewa masuala ya kitaaluma.
VII.
Kuhakikisha kuwa mazingira ya Chuo yanakuwa rafiki
kwa Jumuia nzima ya Chuo na Jamii inayozunguka Chuo;
VIII. Kushauri uongozi wa Chuo na serikali kuhusu masuala
yote itakayoyaona kuwa ni muhimu katika maendeleo ya
Chuo.

Kwa maneno haya ya Mwalimu, serikali inaona kuwa mnao
wajibu si tu kwa chuo bali pia kwa jamii nzima kwa kuhakikisha
kuwa chuo kinakua na kustawi ikiwa ni pamoja na kukitumia
na kukikuza kwa lengo la kuendeleza michezo ili kujenga taifa
lenye afya njema kupitia michezo. Vilevile, kwa kuwa michezo
ni biashara na ajira, siyo tu kwamba tutajenga Taifa lenye afya
njema, bali pia vijana wetu watapata kipato kupitia fani ya
michezo.

Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,

Ni matarajio ya serikali kuwa, ninyi wote pamoja na wadau
wengine wa michezo nchini, mtafanya kila liwezekanalo kuona
Chuo chetu kinapiga hatua kubwa kuelekea huko tunakotaka
kifike.

5

Mh. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, wakati wa ujio wa kombe la Dunia tarehe 19
Novemba, 2009; alisema; nanukuu,” Unatakiwa kuonyesha
mfano, ndipo watu wengine wakusaidia, hapo
utaeleweka, kinyume cha hapo mambo yatakuwa
magumu na kushindwa kupata maendeleo ya kweli”.
Mwisho wa kunuukuu.

Kwa maana hiyo, Bodi hii inalo jukumu kubwa la kuwa mstari
wa mbele katika kuhakikisha kuwa Chuo kinasonga mbele kisha
ndio wengine wafuate katika kukifanya Chuo kujiendesha na
kujitegemea.

Kwa hayo machache, napenda kutamka kuwa Bodi hii ya Chuo cha
Maendeleo ya Michezo Malya sasa imezinduliwa rasmi.

AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA
Axact

Post A Comment: