Maandamano ya nchini misri yasababisha watano kuuwawa na 644 kujeruhiwa
Wanajeshi nchini Misri wameanza kuwafukuza waandamanaji, ikiwa ni pamoja na waandishi wa mashirika mbalimbali ya habari, waliokusanyika nje ya kasri ya rais mjini Cairo.
Hatua hiyo ni kufuatia ghasia za usiku kucha kati ya waandamanaji wanaomuunga mkono Rais Mohammed Morsi, na wale wanaompinga.
Kutokana na fujo hizo, watu watano waliuawa na wengine 644 kujeruhiwa.
Serikali ilikuwa imetangaza kwamba waandamanaji wote walitazamiwa kuondoka kufikia saa 13:00 GMT.
Hayo yakiendelea, shirika kubwa zaidi la waislamu nchini Misri kutupilia mbali mamlaka makuu aliyojitangazia.
Taasisi ya Al-Azhar imemtaka rais, pasipo masharti yoyote, kufanya mashauri na wapinzani wake.
Bw Morsi, ambaye aliingia uongozini nchini Misri kwa kushinda kwa kura chache katika uchaguzi wa kwanza huru nchini humo mwezi Juni, alitangaza kwamba atayatupilia mbali madaraka hayo aliyojikabidhi, mara tu katiba mpya itakapoidhinishwa.
Lakini kumekuwa na malalamiko kuhusiana na rasimu hiyo ya katiba.
Wapinzani wanasema rasimu hiyo iliharakishwa bungeni, pasipo majadiliano ya kutosha, na inadhaniwa haitaweza kuwapa kinga wapinzani wa serikali, na kulinda uhuru kamili wa dini, na vile vile haki za wanawake.
Serikali inasisitiza kwamba rasimu hiyo ya katiba, iliyotayarishwa na jopo ambalo wanachama wake wengi ni waislamu wanaomuunga mkono Morsi, itapitishwa baadaye mwezi huu, licha ya rasimu hiyo kupingwa vikali.
Watu wanne, miongoni mwa washauri wa Bw Morsi, walijiuzulu siku ya Jumatano, katika hatua ambayo inaonyesha wanaupinga uamuzi wa rais huyo.
Washauri wengine watatu walijiuzulu wiki iliyopita, na shirika la habari la Mena lilitangaza siku ya Alhamisi juu ya watu wengine zaidi kujiuzulu
Habari hii nikwa msaada wa Shirika la habari la Uingereza BBC.
Axact

Post A Comment: