Jee unajua kuwa ukikua pua yako na masikio yako pia yanazidi kukua , kurefuka na
kupanuka?
Hebu angalia wazee walio karibu na wewe utaona kuwa pua zao ni ndefu au zimepanuka.
Masikio yao pia ni marefu.
Ni sayansi hiyo!

Jee unajua kuwa macho peke yake ndio hayakui?
Tangu ulipozaliwa hadi sasa macho yako, yako vile vile, ukubwa ule ule.
Macho hayapanuki wala hayakui!
Mifupa ya Maiti Kitandani
......
Kwanini basi masikio na pua vinakua?
Ukweli ni kwamba vyote havikui.
Pua haikui, masikio pia hayakui. Isipokuwa vyote vinavutika!
Pua na masikio huvutika vikielekea chini kadri umri unavyoongezeka!
Wanasayansi wanasema hii ni kutokana na nguvu ya mvuto au Force of Gravity, Mvuto wa kuelekea
ardhini, Force of Gravity!
Hii nguvu ya mvuto kuelekea ardhini au force of gravity ni mbaya sana!
Nguvu hii ya asili ndio hufanya , nyama mwilini ikavutika au kusinyaa na macho kuonekana madogo.
Ukubwa wa macho ni ule ule bali yanaonekana madogo kwa sababu yameingia ndani kutokana na
kuvutika kwa nyama kwenye uso wako, au sura yako.
Ukweli ni kwamba jinsi ulivyozaliwa macho yako yanasalia kuwa na ukubwa au udogo ule ule.
........
Nguvu ya mvuto ni mbaya!
Ni nguvu hiyo ya Force of Gravity inafanya matiti ya wanawake kurefuka na kukosa ule umaridadi wake.
Sehemu nyeti za wanaume, sehemu za surualini pia hurefuka na kulegea kutokana na force of gravity,
nguvu ya mvuto, mvuto wa kwenda ardhini.
Ardhini ulitoka na Ardhini utavutwa na kurudi huko,
............
Mwanadamu ni kiumbe cha ajabu, kiumbe pekee, kiumbe kilicho barikiwa.
Wewe ni waajabu.
Asubuhi urefu wako huongezeka kwa sentimita moja.
Jua linavyopanda na wewe ukiendelea kuhangaika au kushughulika ,urefu wako nao unapungua kidogo
kidogo.
Ifikapo jioni urefu wako huwa umepungua kwa sentimita moja.
.......
Wanasayansi wanasema kupungua au kuongezeka kwa urefu wa mwanadamu unatokana na gegedu
kwenye miguu na magotini.
Gegedu, kwa kimombo ni cartilage , gegedu ni sehemu ipatikanayo mwishoni mwa mifupa ya miguu
hasa kwenye magoti. Kwa wapendao nyama hii ni mifupa laini inayotafunika. Jua likipanda, magegedu
magotini nayo yana nyauka au kufinyika na kupunguza urefu wa mtu.
.......
Jee unafahamu kuwa asilimia 41 ya wanawake hawazungumzi na mama wakwe zao. Mothers- in-law,
Asilima 41 hawana mahusiano mazuri na mama za wabwana zao. Hawazungumzi nao.
Utafiti unaonyesha kati ya wanawake 10, mmoja wao ana ugomvi na mama mkwe wake.- mother-in-law.
Utafiti uliofanywa na shirika la OnePoll la Uingereza unaonyesha kuwa ugomvi mkubwa kati ya mama
mkwe na wake za vijana wao ni kutokana na usemi maarufu " sisi zama zetu tulikuwa tunafanya hivi au
vile " .
Wanawake hawataki kuambiwa zama zile au kukosolewa mara kwa mara.

Utafiti huo pia unaonyesha kuwa nusu ya wanawake, washawalalamikia mabwana zao kuhusu kina mama
zao, wazazi wa bwana wa kike.
Asilimia 15 ya wanawake wamewahi kukosana , ndoa kuvunjika kutokana na ugomvi kati ya mkwe na
mama mkwe.
Ugomvi mkubwa zaidi kati ya mke na mama mkwe kuhusu malezi ya watoto, wajukuu.
..........
Axact

Post A Comment: