SUALA LAKUWAWEZESHA WAJASIRIA MALI NI JAMBO AMBALO MKUU WA MKOA ALILITOLEA MAELEZO, NA JINSI MKOA ULIVYOPIGA HATUA.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amewaambia waandishi wa habari jijini hapa, kuwa kama tunafanya vizuri katika maendeleo, basi tusibeze jitihada za serikali, kwani kufanya hivyo nikuwapotosha wananchi.
Aliyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari jini hapa siku ya tarehe 29.12.2012.
Ndikilo alisema kumekuwepo na baadhi ya waandishi wa habari wasio itakia mema nchi na badala yake kuandika vitu kana kwamba hawaoni kinacho tendeka na Serikali.
Ndikilo alikuwa akitoa tahtmini ya utendaji wa Shughuli za serikali kwa kipindi cha 2005-2012. baadhi ya nyanja alizo zigusia ni alisema pato la mwanza Mwanza limekuwa kutoa kiasi cha Tsh. 400000 mwaka 2005  hadi kufikia Tshs 900,000 mwaka 2012., haya ni mafanikio sio yakubeza ndugu zangu.

VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI VIKIFATILIA KWA MAKINI MAELEZO YA MKUU WA MKOA WA MWANZA TARE. 29.12.2012, JIJINI MWANZA
Alisema pia kuwa Mkoa wa Mwanza ni mchangiaji mkubwa wa pato la Taifa ambapo kwa mwaka 2011 Mkoa ulichangia asilimia 9  ukiwa ni Mkoa wa pili ukitanguliwa na Mkoa wa Dar es Salaam uliochangia asilimia 16.6.
Mkoa umekuwa ukisimamia mashindano ya kilimo kupitia maonesho ya kilimo yanayofanyika kila mwaka. Mwaka 2012 ni mwaka wa tano tangu Mkoa uanze kuadhimisha sikukuu ya wakulima na maonesho ya kilimo.
 Katika maonesho haya wakulima hushindanishwa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Wilaya, wakulima bora wanaozingatia kanuni bora za kilimo cha mazao mbalimbali ndio huletwa ngazi ya Mkoa. Katika ngazi ya wilaya hushindanishwa ili kupata wilaya ambayo wakulima wake wametekeleza ipasavyo kanuni za kilimo. Pia Mkoa kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba, umekuwa ukishindanisha wakulima wa zao la pamba kuanzia ngazi ya kijiji hadi Mkoa. Wakulima wanaofanya vizuri huzawadiwa trekta dogo la mkono (Power tiller), mabati na baiskeli. Wakulima waliofaidika na utaratibu huu wa mashindano tangu 2005/2006 hadi 2010/2011 ni 51.

MWANDISHI WA GAZETI LA SERIKALI BW. NASHON KENNEDDY ALITAKA KUJUA NINI HATIMA YA MASULA YA USHIRIKA, NA ZAO LA PAMBA
Mbali na masula ya Kilimo Mkoa vilevile umefanya vizuri katika Uvuvu, Ufugaji, Miundombinu, Ujasiriamali, ushirika, Masuala yakuwapatia wananchi maji safi na salama, Huduma za Afya, Elimu,n.k.


MGANGA MKUU WA MKOA WA MWANZA DR. VALENTINO BANGI HAPA AKIPATA NUKUU MUHIMU WAKATI WA KIKAO HICHO
Axact

Post A Comment: