Na Atley Kuni.
Katika kile kinacho onekana kuwa ni dhana ya uchapakazi, wataalamu kutoka Sekretariti ya Mkoa wameanza kazi kwakwenda kutembelea Wilaya za Mkoa huo nakufanya Tahthmini ya Shughuli, mbali mbali zinazo tekelezwa na serikali katika halmashauri.
Kwamujibu wa taarifa iliyopatika kutoka kwa baadhi ya wataalamu hao, ziara za kutembelea Miradi mbalimbali ya maendeleo  ni pamoja na kufanya thamini ya utendaji wa Halmashauri kwakuzingatia dhana ya Utawalabora.
Timu inayo ongozwa na Mwl. Hamis Maulid ambayo ilipewa jukumu la kwenda kufanya shughuli zake katika halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kati ya tarehe 17/12/2012 na tarehe 22/12/2012, wakiwa Wilyani humo wataalamu hao walipata fursa yakutembelea miradi ya Ujenzi wa Bwawa kwaajili ya kilimo cha Umwagiliaji la Mahiga ambalo hadi kukamilika kwake linatarajiwa kugharimu kiasi cha Tshs Bilioni I.9 nakuona mwenendo mzima wa ujenzi wa bwawa hilo.
Akitoa maelezo Mhandisi wa Maji   bibi Magreth  Kavalo alisema ujenzi wa Bwawa hilo unatazamiwa kutoa, huduma ya Umwagiliaji wa mashamba ya mpunga  kwenye vijiji vipatavyo vitatu vya Ngudulugulu, Mahiga na Mwang'halanga hadi kukamilika kwake.
Mara baada yakutembelea mradi huo mkubwa kabisa ambao unatekelezwa chini ya Serikali ya awamu ya nne, wataalamu hao washauri walitembelea, mradi wa maji wa Mwabaratuli, Mradi wa maji Isingisha, kukagua barabara iliyojengwa kwa kiwango cha changarawe, mradi wa Uchakachaji wa Mazao ya ngozi, nyumba za watumishi za daraja A,ujenzi wa Bweni la Waschana katika shule ya Sekondari Bujiku Sakila, pamoja na Ukaguzi wa Ujenzi wa Wodi ya kulaza wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Ngudu ya daraja la II.
Mbali ya ukaguzi wataalamu hao pia walipata fursa yakuzungumza na wataalamu washauri katika, halmashauri hiyo kusikia changamoto zinazo wakabili katika kufanikisha malengo yao ya utendaji kazi.
 Desemba tarehe 03/12/2012, Kikao kilicho keti Ofisini kwa Katibu Tawala wa Mkoa huo Bibi Doroth Mwanyika, Kikao hicho cha  Menejimenti cha Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, kiliazimia kufatilia nakufanya tathmini ya Utendaji kazi wa Shughuli za Serikali katika hamashauri za Wilaya za Mkoa huo.
Kwamujibu  wa wa Sheria namba 19 ya Mwaka 1997, Sekretariti za Mikoa ndizo zenye jukumu la Kusimamia na kuelekeza kitaalam Utendaji wa shughuli za Halmashauri za Wilaya.
Mkoa wa Mwanza ni mmoja kati ya mikoa 25 iliyopo Tanzania bara na Mkoa pekee wenye kukua  kwa kasi kutokana na muingiliano wa shughuli za kibiashara, zinazo endeshwa mkoani humo hasa ikizingatiwa umekuwa kitovu na lango la biashara kwa nchi za Afrika Mashariki na kati.
Axact

Post A Comment: