Somalia
Ujumbe wa juu kutoka serikali ya Somalia ulikutana na kiongozi wa wapiganaji wa Ras Kamboni Sheikh Ahmed Mohamed Islam huko Kismayu Alhamisi (tarehe 27 Disemba), Redio Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa iliripoti.

Islam alisema kutokubaliana kati ya utawala wa muda wa Kismayu na serikali ya Somalia kumesuluhishwa. “Tunaelewana vizuri na serikali ya shirikisho,” alisema.
Ujumbe ulijumuisha Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa Abdikarim Hussein Guled, Waziri wa Ulinzi Abdihakim Haji Mohamud Fiqi na Waziri wa Mawasiliano Abdullahi Ilmoge. 
Abdinasir Serar, msemaji wa jeshi la Ras Kamboni, alisema pande mbili zilikubaliana kuunda utawala mpya kwa mikoa ya Jubba kulingana na katiba ya nchi na kujumuisha jeshi la Ras Kamboni katika jeshi la Somalia.
“Tulijadili masuala ya kijeshi na jinsi watu wa mkoa wa Jubba wanaweza kusaidiwa,” Serar alisema.

Chanzo: Mtandao wa Sabahionline.Com
Axact

Post A Comment: