Tume ya uchaguzi ilisema kuwa bwana Mahama alishinda kwa asilimia
hamsini na saba ya kura na kuondoa uwezekano wa kufanyika duru ya
pili ya uchaguzi huo dhidi ya mpinzani wake Nana Akufo-Addo aliyepata
asilimia 47 ya kura.
Chama cha upinzani New Patriotic Party, kimedai kutokea wizi wa kura na
kusema kitafanya mkutano hapo keshi kuamua hatua watakazochukua.

Ghana imejipa sifa ya kuwa nchi yenye demokrasia thabiti barani Afrika na
moja ya nchi zinazokuwa kwa kasi kubwa barani Afrika.
Kwa upande wake rais Mahama aliwataka watu kuheshimiana kufuatia
matangazo ya kura ambayo yalimpa ushindi.

Hapakuwa na ripoti zozote za ghasia Jumatatu asubuhi baada ya
matangazo ya uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali kutangazwa siku
ya Jumapili.
Axact

Post A Comment: