Mkoa wa Mwanza unatarajia kufanya uzinduzi wa Chanjo ya  Kimkoa kuhusu Nimonia pamoja na Kuzuia kuhara kwa watototo wenye umri wa wiki sita hadi  Mwaka mmoja.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr. Valentino Bangi, amesema uzinduzi huo utakufanyika Tarehe 02. Januari 2013, kwenye Wilaya ya Sengerema katika kijiji cha  Sima na Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Mheshimiwa wa Mkoa wa Mwanza  Mhandisi Evarist Ndikilo. Lengo la chanjo hiyo nikuhakikisha watoto wote wenye  Umri wa wiki sita hadi mwaka mmoja wanapata chacho hiyo ili kunusuru watoto na maradhi ambayo wanaweza kuyapata, ameuambia mtandao huu kuwa Ujumbe Mahsusi wa siku hiyo ni:   Jamii iliyo chnjwa ni jamii yenye Afya.
Kaulimbiu  katika siku hiyo ni kuwa  kutochanjwa kwa mtoto ni hatari kwa mtoto mwenyewe lakini vilevile watoto wenzake atakao kuwa anashirikiana nao.
Mkoa wa Mwanza   ni mmoja kati aya Mikoa ya Tanzania bara na upo mbele katika Jitihada za kuhakikisha Nchi inakuwa na jamii yenye ustawi kwa wananchi wake.

IMEANDIKWA NA:  ATLEY KUNI, MWANZA.
Axact

Post A Comment: