Na Alex Mchumvu. Tanga.
Baadhi ya watoto wanaoshambuliwa na ugonjwa wa funza. Kuanzia mtoto
wa pili kutoka kulia ni miongoni mwa familia zinazoshambuliwa na
ugonjwa wa funza eneo la Kibaoni Korogwe Vijijini.

Hata hivyo si watoto wa familia zote wamekubwa na ugonjwa huo, wapo
ambao wanaangaliwa kwa karibu na familia zao kama wanavyoonekana
baadhi ya watoto katika picha hii, ambao wamesalimika. Funza Korogwe
Vijijini BAADHI ya watoto wanaokosa uangalizi wa karibu kutoka
kwa wazazi au walezi wao wamekubwa na ugonjwa wa kushambuliwa
na funza kwa kiasi kikubwa miguuni na mikononi hali iliyosababisha
kuharibika kwa miguu yao na mikono kiasi kikubwa. Idadi kubwa ya
watoto walioathiriwa na wadudu hao wameonekana katika eneo la Kibaoni
Korogwe vijijini, ambapo baadhi walipohojiwa na Thehabari walizitupia
lawama familia zao kwa kutowaangalia kwa karibu kiasi cha kushambuliwa
na funza. Kassim (si jina lake sahihi) anasema nyumbani kwao watoto
wote wameshambuliwa na funza kuanzia miguuni hadi mikononi hali
ambayo imewanyima kuwa huru katika kujumuika na wenzao. “Wadudu
hawa wanawasha na kuleta maumivu makali kiasi ambacho hushindwa
hata kujumuika nawenzako…huwa najaribu wapunguza na kumsaidia
mdogo wangu pia lakini wanatuzidi ni wengi,” anasema mtoto huyo. Hata
hivyo mbali na maumivu na kuwashwa mfululizo, mikono ya kijana huyu
imeshambuliwa vibaya na funza kiasi kinachomnyima uhuru wa kuitumia
mikono vizuri kushikia vitu anuai kutokana na maumivu. Ardhi ya kibaoni
ni ya udogo mwekundu wenye vumbi hasa kipindi cha kiangazi. Baadhi ya
watu wanasema wadudu aina ya funza wanaoshambulia binadamu ustawi
zaidi katika mazingira machafu na yenye vumbi kiasi kikubwa. Watoto na
hata watu wanaoshambuliwa na wadudu hao wanaishi katika mazingira
kama hayo.
Axact

Post A Comment: