Ni kuhara na Kichomi kwa watoto wa wiki 6 hadi mwaka mmoja.
Zoezi la Chanjo limefanyika kimkoa katika Wilaya ya Sengerema kwenye Tarafa ya Sengerema
kijiji cha Sima na Kata ya Sima Mkoani Mwanza.

Akizindua zoezi hilo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo amesema zoezi
hilo kimkoa ni lazima lifanikiwe kwa mujibu wa malengo walio jiwekea ya 95% kwa kila wilaya
kinyume chake wale wote watakaoshindwa kufikia lengo itabidi wajieleze na sababu zilizofanya
washindwe kuvuka malengo katika Mkoa wake.
Ndikilo amesema yeye kama mtendaji Mkuu katika Mkoa wa wa Mwanza hayupo tayari kuona
Mkoa huo unakuwa wa mwisho katika zoezi hilo.
Amewahimiza wazazi kujitokeza kuhakikisha watoto wao wanapatiwa chanjo hiyo kwani kuacha
kuwachanja watoto, si hatari kwa mototo tu, bali pia watoto wenzake wanao mzunguka hivyo ni
vema kila mzazi akaona umuhimu wakumpeleka watoto katika chanjo.
Mkuu huyo wa Mkoa amewahakikishia wananchi wa Sengerema na Mkoa wa Mwanza kwa
ujumla wake kuwa, chanjo hiyo ni salama kwakuwa imefanyiwa utafiti wakutosha na wataalam
wa afya wa Ulimwenguni na Wizara ya afya hapa nchini.
Akihututubia mamia ya wananchi wa kijiji hicho cha Sima, Amesema watoto wa chini ya miaka
5 wanachangamoto nyingi, hasa kwenye nchi zetu hizi zinazo endelea , kwani kwingineko kwa
nchi zilizo endelea watoto wanao zaliwa hukua kwa takriba ni 99% tofauti na hapa kwetu.
Amesema ugonjwa wa kichomi huua watoto kwa 14% ukitanguliwa na Malaria ambao huuwa
kwa asilimia 15% huku ugonjwa wa kuharisha ukishika nafasi ya tatu kwa kuuwa watoto wengi
kwa asilimia 12% kwani nchini Tanzania kila mwaka watoto walio chini ya umri wa miaka
mitano wapatao takriba ni 198,443 huugua ugonjwa wa kuharisha na kati yao 13,397 hufariki
dunia.
Ujumbe mahususi wa siku hiyo ni Jamii iliyochanjwa ni Jamii yenye afya, ameongeza kuwa
Chanjo hiyo ni sehemu ya Ilani, hivyo kufika 2015 jamii ya kitanzania iwe ni jamii iliyo na
ustawi.
Magonjwa ambayo hadi hivi sasa yana chanjo ni donda koo, kichomi, kuharisha, pepopunda,
kifua kikuu, surua, homa ya uti wa mgongo, kifaduro, homa ya ini, na polio, haya ndio
magonjwa yaliopo katika mpango wa Taifa wa chanjo alisema na kuongweza.
Amehiza viongozi wa kila ngazi kuzindua kampeni hiyo, na watoto walengwa ambao ni kuanzia
wiki 6 hadi wiki 32 wapatiwe chanjo hiyo bila kukosa.
Jumla ya watoto 149,000 wanategemewa kupatiwa chanjo hiyo na amesema zoezi hilo ni
endelevu hadi tarehe 31. DEC. 2013.

Kaulimbiu ya katika maadhimisho hayo ni kuwa “Mtoto asiye chanjwa ni hatari kwake
na kwawenzake, mpeleke mototo wako akachanjwe”.

Imeandaliwa na
www.kuninews.blogspot.com

Na Atley Kuni.


PICHA ZAIDI ZA UZINDUZI HUO



Axact

Post A Comment: