Na Afisa habari RS Mwanza.

Kikao cha kamati ya ushauri cha mkoa (RCC), kitafanyika tarehe 08.Januari 2014 ili kuweza kujadili mambo mbali mbali ya Maendeleo katika mkoa huo.

MKUU WA MKOA MHANDISI  EVARIST  NDIKILO.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo mtandao huu imezipata ni kwamba pamoja na mambo mengine, kikao hicho pia kitajadili maendeleo ya mkoa huo katika Nyanja tofauti tofauti kama bara bara, muelekeo wa hali ya uchumi wa mkoa na mfumuko wa bei, suala la elimu, kilimo, mifugo biashara na ushirika.

Lakini pia katika kikao hicho itakuwa ni fursa pekee ya kujadili maendeleo ya Matokeo makubwa sasa (BRN), maendeleo ya zao la Pamba, Upandishwaji hadhi kwa baadhi ya miji, Rushwa na maadili yaViongozi lakini pia kuona njia bora katika kuinua Uchumi wa Mkoa.

RCC Ndicho kikao kikubwa kabisa katika Ngazi ya mkoa ambapo wajumbe wake ni pamoja na Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mwenyekiti, Katibu Tawala wa Mkoa ambaye ni Katibu, na wajumbe wengine wanao unda kanmati hiyo ni Wabunge, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Mameya wa majiji na manispaa.

Katika kikao hicho pia huwahusisha wataalam washauri wa Sekretarieti ya Mkoa pamoja na Wachumi wa Wilaya.
Axact

Post A Comment: