Serikali Mkoani Mwanza imeamuru shule 11 za msingi  na moja ya Sekondari, zilizokuwa zimefungwa Wilayani Ukerewe kutokana na ukosefu wa vyoo zifunguliwe na wanafunzi warejee kwenye masomo wakati wa  hatua za dharura zinachukuliwa.

 

Hatua hiyo imefikiwa mapema hivi leo wakati wa kikao cha pamoja baina ya uongozi wa  Mkoa na Wilaya kukaa na kuangalia hatua zipi zifuate mara baada ya hapo jana Mkurugenzi wa Wilaya ya Ukerewe Bw. Frank Bahati, kukieleza kikao cha Ushauri cha mkoa wa Mwanza kuwa, wamezifunga shule hizo kutokana na kukosa vyoo.

 

Aidha pia  halmashauri ya Wilaya imeelekezwa kuwatumia watendaji wa kata na Vijiji,  kusimamia zoezi hilo na kuwahamasisha wananchi waweze kushiriki katika kufikia adhma hiyo ya ujenzi wa vyoo ili wanafunzi hao waondokane na adha inayo wakabili.

 

Kwa upande wa Uongozi wa  halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, umeahidi kutenga kiasi cha Mil.80 kutoka katika makusanyo ya  ndani kwaajili yakufanikisha zoezi hilo la dharura, huku Wananchi wakitakiwa kushiriki katika uchimbaji wa mashimo.

 

Shule za msingi zilizokuwa zimefungwa kutokana na kukosa vyoo ni pamoja na Muhuzya na Murutanga za kata ya Bukindo, Busangu na Mugu za kata ya Namilembe, Buzegwe na Kilongo za kata ya Kagunguli, zingine ni Mukasika na Muhandi za kata ya Murutunguru, Mubule iliyopo kata ya Nyamanga na Chankamba iliyopo kata ya Igalla.

 

Wakati kwa upande wa Sekondari ni shule moja tu ya Lugongo iliyopo kata ya Murutunguru.

 

Imetolewa

Atley J. Kuni
AFISA HABARI RS MWANA

Mwanza

 
Axact

Post A Comment: