Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo kwa Wakulima nchini akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella mapema kabla ya makabidhiano hayo kwenye eneo la tukio(Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa mkoa)
Wakulima wa mkoa wa kanda ya ziwa kwa ujumla wameshukiwa na neema ya pekee kufuatia jitihada za serikali ya awamu  tano kuwaanzishia Benki yao katika kanda hii, ambayo itakuwa na makao yake makuu katika Mkoa wa Mwanza.



Makabidhiano ya funguo yakiendelea baina ya Meneja wa Wakala wa majengo Mkoa wa Mwanza Eng. Yohana Mashausi na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo nchini ndugu Francis Assenga, huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mwenye kofia akishuhudia tukio hilo.

Jengo hapa likifunguliwa tayari kukaguliwa na kukabidhiwa kwa wahusika.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akizungumza wakati wa makabidhiano wa jengo litakalo tumika kwa ajili yashughuli za kibenki kwa kanda ya ziwa lakini pia kama tawi kwa mkoani wa Mwanza, amesema Sekta ya kilimo ambayo hubeba zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa Tanzania kwa sasa imepatiwa mkombozi.

“Kama mnavyo fahamu, sekta hii ina mnyororo mrefu, wapo wanao lima, wengine wanachakata mazao lakini wapo pia wanao safirisha mazao kwendanje ya nchi na wengine wanao leta mzao ndani ya nchi, alisema Mongella na kuongeza, “tunavyozungumzia asilimia 80% ni hawa wote, tunataka mwisho wa siku kilimo kimlipe mtu na kuendesha maisha yake” alisema Mkuu wa Mkoa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Kilimo Nchini, Francis Assenga, yeye amesema shabaha yakufunguliwa kwa benki hiyo nikutaka kumkomboa mkulima kutoka katika kilimo cha kujikimu na kuingia katika kilimo cha kibiashara, “Tukasema tuangalie sehemu ambayo inamatokeo ya haraka lakini eneo ambalo linachangia kwa kiwango kikubwa katika pato la taifa, tukasema Mwanza ni mahali sahihi”. Alisema Assenga.

Amesema kanda ya ziwa inayo miradi mingi ya kilimo hasa wingi wa  viwanda ambavyo vitatumika, katika kusindika , kuchakata na kufanya kilimo cha biashara ambapo mnyororo wa thamani ulivyo kwa kanda ya Mwanza.

Mkurugenzi huyo, amesifu pia utayari wa Viongozi wa Mkoa wa Mwanza wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa kwa utayari walio uonesha lakini pia kutafuta eneo ambalo Benki hiyo itakuwepo, “Kimsingi tumefurahishwa sana na utayari wa Mkuu wetu wa Mkoa John Mongella, akisema anatenda, sasa miongoni mwa kanda sita tunazo kwenda kuzianzisha Mwanza inakuwa kanda ya kwanza kwani fedha tayari zimetolewa na serikali kwa ajili ya uanzishwaji wa Benki hii” alisema Assenga.

Katikati ya Makabidhiano hayo, Mhandisi wa Majengo katika Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Yohana Mashausi, akasema wao wapo tayari kwaajili yakuwakabidhi Benki ya wakulima Jengo ambalo lilikuwa likitumiwa na Mamlaka ya mapato (TRA) hapo kabla.

Mwandishi wa habari kutoka Magazeti ya serikali Nashonny Kennedy, akitaka uafanuzi wa jambo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Wakulima nchini, wakati wa hafla ya Makabidhiano ya Benki hiyo.
Axact

Post A Comment: